TOBO LA PANYA (65)

SEHEMU YA SITINI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NNE: Safari ni ndefu kidogo, ambayo inavuka vyumba kadhaa, kabla ya kuishia kwenye mlango mmoja mzito wa chuma, wenye kidirisha kidogo sana, tena lipo kwa juu, na limezibwa kwa kioo kizito. ….ENDELEA…….

Yule koplo anafungua mlango na kuingia ndani, ambako tunawakuta watu wawili, yani askari wa jeshi la polisi mwenye alama ya nyota moja beganio mwake, akiwa amekaa kwenye kiti, kilichopo nyuma ya meza kubwa ya chuma, huku mbele yake akiwa kijana mmoja raia kwenye kuvaa nguo zilizo chafuka kwa damu nyingi sana, alie kaa kwenye kiti cha chuma, pingu na minyororo ikiwa imeshika mikono na miguu yake.

Wote wanatazama upande wa mlango, sura zao zinakagawanyika katika mionekano miwili, wakati yule afisa wa polisi mwenye cheo cha A-Insp anatoa macho ya mshangao, huku mtuhumiwa anaachia tabasamu pana.

“afande ni mawakara wa TSA, wanamwitaji mtuhumiwa” anasema asari koplo, na hapo yule afisa anamtazama huyu mtuhumiwa mbele yake, ambae anamwonyeshea mikono kwamba amfungue zile pingu.

Nikama yule afisa wajeshi la polisi, amechukia hivi, maana anasimama ghafla, na kuingiza mkono mfukoni, anatoa funguo na kuziweka mezani, “koplo mfungue” anasema yule afisa wa polisi, huku anatoka nje na kutokomea kwenye kolido.

Dakika chache baadae wanaonekana wale wanausalama, wakiwa wanatoka nje ya jengo wameongozana na huyu mtuhumiwa, na kuingia nae ndani ya gari, aina ya mercidise benz, kisha gari linaanza kutembea taratibu, kuelekea nje ya geti.

Wanapishana na gari dogo aina ya BMW jeusi, ambalo linaenda kusimama mita ishilini toka getini, ndani ya BMW kuna watu wawili, yani Insp Aisha Amary, aliekuwa na mwanaume kijana mdogo, ambae licha ya kumwokoa toka kwenye mikono ya Nyondo, lakini hakuwa anamfahamu jina.

“sasa unaweza kushuka, hakikisha unakaa katika ulinzi” alisema dereva wagari lile, ambae ni kijana Hance, “samahani kaka, naomba nikufahamu” alisema Insp Aisha, kwa sauti ya kubembeleza, huku anaachia tabasamu laini.

“ni hatari kwako, sababu muda mfupi ujao utapewa jukumu zito ambalo, linaitaji huruma yangu, ili uendelee kuwa hai” alisema Hance kwa sauti tulivu, huku anatazama mbele.

“lakini siyo kaajili ya kazi, nikwaajili yangu binafsi” alisema Insp Aisha, huku anaendelea kuachia tabasamu la kirafiki, “lakini bado ni polisi, na unaitaji kutoa maelezo yenye umakini wahali ya juu kwa viongozi wako, yanayo nihusu mimi” alisema kijana Hance.

Hapo nikama Insp Aisha anaingiwa na simanzi kidogo, “sikia kaka yangu, kwa sasa wewe ni mtu muhimu kwangu, kwamsaada ulio nipatia leo, sitojisikia vizuri kama nikikupoteza” alisema Aisha, kwa sauti iliyo nyongea, huku anamtazama hancekwa macho ya huruma.

Hance anamtazama Aisha, nikama anajiuliza kuwa huyu mwanamke anamaana gani, anamwona anamtazama kwa macho ya huruma, inamshangaza Hance, aelewi huyu mwanamke kwanini anakuwa hivi.

“sikia dada mimi nilienda pale kwa inshu nyingine kabisa, nikaamua kuachana na mambo yangu kukuokoa wewe, sasa mbona unataka kuwa chanzo cha kuanguka kwangu” anauliza Hance kwqa sauti tulivu yenye usikivu makini.

“hapana kaka, mimi sina maana hiyo, mimi nakutaka wewe ambae umeniokoa, usijari umri wangu, mimi bado sijaolewa, unaweza kufaidi kile ulicho kiokoa, kwa namna yoyote, ata kama uitaji kuniowa” alisema inap ahaisha huku anainamisha kichwa kwa aibu.

Hance anashusha pumzi nzito, misiri ya mtu alie hoshwa na jambo na asijuwe la kufanya, “ok! dada yangu, nitakutafuta baada ya ya aya yote kuisha” alisema Hance na hapo Insp Aisha anaachia tabasamu pana, huku anamtazama Hance.

Aisha anamwona kijana mpole, namwona anamtazama kwa macho tulivu, huku anaachia tabasamu, Aisha anasogeza mdomo wqke kwenye shavu la Hance na kumpa busu matata, la kulamba shavu lake, kisha anamwachia, huku Hance mwili unamsisimka.

“naamini mtu makini kama wewe, unasimamia ahadi zako” alisema Aisha huku anafungua mlango na kutoka nje ya gari, “usijari jiandae kukutana, baada ya kesho kumaliza kila kitu” alisema Hance huku kabla ajakanyaga mafuta na kuondoa gari, kuelekea mashariki mwa mji wa Songea.

Insp Aisha analitazama gari likiondoka, huku anavuta picha ya tukio la uokozi wake, uliotokea wakati akivuliwa nguo, tayari kubakwa kwa mtungo wa vijana watatu.

Insp Aisha anatabasamu kidogo, “mh!, sijuwi ingekuwaje” anajisemea Aisha, huku anaanza kutembea kuingia ndani ya geti la makao makuu ya jeshi la polisi.

Pale nje ya jengo la makao makuu, Insp Aisha kwambali, anaona askari wamekaa kwa vikundi wanajadiri jambo, Aisha anaishi wanajadiri kutekwa kwake, “usikute wanahisi nimeenda kubakwa” anawaza Insp Aisha, huku akimshukuru kijana mpole ambae amemwokoa toka kwenye aibu ile.

Lakini kabla ajawafikia wale askari wenzake, akaona msururu wa magari yakiingia pale makao makuu ya jeshi la polisi, likiwepo gari la RPC, staff officer, RCO na gari lwenye polisi kadhaa likiwa nyuma kabisa, Insp Aisha anakumbuka kuwa, aliwaona wakina RPC kule msibani, nyumbani kwa mzee Nyondo. . ….*

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!