TOBO LA PANYA (67)

SEHEMU YA SITINI NA SABA

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA SITA: “unazani sasa hivi tutapata usafiri gani?” anauliza Rose kwa sauti ya chini, “ilakweli, sas ivi hakuna dala dala” anaunga mkono Hidaya, kwamba swala la kuondoka mida hii, lilikuwa gumu kwa upande wao. . ….ENDELEA

“sijuwi yupo wapi yule shetani, alafu ata watu wake siwaoni” anasema Rose, huku anatazama kwenye kiti ambacho mwanzo, alikuwa amekaa Nyondo mwenyewe, “nazani kuna kitu wanafanya, siuliwaona wale polisi” alisema Hidaya, huku nae anatazama upande ule ule wenye kiti cha bwana Nyondo.

Kitu ambacho siyo wakina Rose peke yao, ila watu wote pale msibani awakujuwa, kinachoendelea upande wa nyuma wa jengo ilikubwa la kifahari, linalomilikiwa na bwana Nyondo.

Naaaam!, ndani ya chumba cha pili toka banda lenye mbwa wakali,ambao sasa walikuwa wanabweka mfululizo, tuna waona watu kumi na nane, miongoni mwao akiwepo bwana Nyondo na kijana wake Kichondo.

Ndani ya chumba vijana kumi na sita kila mmoja ameshika bunduki aina ya AK-47, kila mmoja akiiandaa kivyake, maana wapo walikuwa wanapakia risasi kwenye mikebe, wapo waliokuwa wanakagua silaha yenyewe.

“nataka mji unuke damu, mpaka huyu mjinga apatikane” alisema Nyondo kwa sauti yenye hasira na ghadhab kali sana, “nina mtaka akiwa mzima, na ikitokea mume muuwa, basi afe kifo kibaya akijapata kutokea” alisema tena Nyondo, huku anawatazama vijana wake, ambao walikuwa wanaendelea na maandalizi yao.

“sitaki kusikia habari ya polisi, maana wao wameshindwa kazi yao, na kama wakijipendekeza wapigeni risasi, alisisitiza Nyondo kwa sauti ile ile, ambayo ukipata bahati ya kuisikia, ungejuwa Nyondo amekasirika kiasi gani.

Iki ni kikundi cha uharifu cha bwana Nyondo, ambacho ukitumia kuteka magari na makubwa, au kuiba spare za magari makubwa yaliyo pata ajari, wakati mwingine utega vikwazo ambavyo usababisha ajari izo.

“boss usiwe na shaka, huyo dogo lazima apatikane, iwe isiwe, lazima apatikane, na tutamlete mzima, japo anaweza kuwa katika hali mbaya” alisema mmoja kati yao, ambae licha ya kubwa na mwili mkubwa, pia alikuwa na ndevu nyingi zilizo zunguka mdomo wake.

“timiza maneno yako Manda, nazani unafahamu umuhimu wa kukamtwa kwa huyu mshenzi” alisema Nyondo kwa sauti ambayo ilianza kushuka kidogo tofauti na mwanzo.

“nakuletea kama alivyo boss, hatujawai kushindwa, sembuse mtu mwenyewe mmoja” alisema huyu jamaa alie itwa Manda,kwa sauti ya kujiamini, “sawa, mimi nasubiri taarifa” alisema bwana Nyondo, klisha akatoka nje nje, akifwatiwa na Kichondo.

Naaaaam!, ili ni moja kati ya makundi hatari sana ya kiarifu, kundi lililotekeleza matukio mengi ya kikatili, likiwepo tukio la kuwa abiria, hamsini waliokuwepo kwenye gari kubwa la mizigo, na kuchukuwa kila kitu, kuanzia mali za abiria, na vifaa vya gari.

Sasa bwana Nyondo anaamua kulitumia kundi ili, baada ya kundi lake la kwanza la kiarifu kuuwawa lote, ikiwa bado anauitaji wa kumpata muuwaji huyu, “Kichondo, hivi huyu mtu ninani, anae thubutu kukuingia kwangu nakuuwa vijanawangu?” anauliza Nyondo wakati wanatembea kuelekea ndani, ya nyumba kubwa.****

Naaaaaaam!, turudi makao makuu ya jeshi la polisi, kanda ya kusini, ambako pale getini tunapishana na gari la polisi, lwenye askari kadhaa, wenye bundi, walio kata kushoto, kuelekea nyumbani kwa ASP Ayoub Mzee, kwenda kushukuwa familia yake.

Nje ya jengi kuu la makao makuu ya jeshi ili, licha ya kuwepo askari wengine, lakini pia tunamwona Insp Aisha, akiwa na ASP Ayoub Mzee, wanapeana habari ya jinsi tukio la utekwaji lilivyokuwa.

“yani afande nikasema tayari nimesha zalilika, ujuwe walishaanza kunivua nguo, bila yule kijana kutokea, sijuwi ningeweka wapi sura yangu” alisikika Insp Aisha akiongea kwa sauti yenye hisia za malalamiko.

“yani jamaa anaamini kuwa, sisi tume mtuma aje kukuokoa, na hivi ameahidi kuniuwa, mpaka ifikapo kesho asubuhi” alisema ASP Ayoub Mzee, kwasauti iliyojawa nawasi wasi mwingi.

“kwahiyo wakuu wanasemaje?” aliuliza Insp Aisha, “wameingia ofisini kwa RPC, kuna jambo wanaenda kuongea, kama ulivyoona, wamesha tumwa askari kwenda kumchukuwa mama Farid na watoto, wanatakiwa wakae hapa mpaka mpaka iliswala lipate ufumbuzi” anaeleza ASP Ayoub Mzee.

“ni mshenzi sana, yule Nyondo, hii yote ni sababu tulionyesha kumwogopa toka mwanzo” alisema Insp Aisha, akionyesha kuchukizwa na matendo ya bwana Tino Nyondo, na maamuzi ya viongozi wake, ambayo siku zote uwazuwia kupambana na mtu huyo.

“vipi yule dogo hatari, umebahatika kujuwa anaishi wapi?” aliuliza Ayoub Mzee, ambae anafahamu fika kuwa moja ya kinacho zungumziwa ndani, na wakuu wao wangazi za juu, ni kumpata yule kijana muuwaji, ambae muda mfupi uliopita amewasaidia kumwokoa askari mwenzao, yani Insp Aisha.

“mh!, yani nikijana waajau kidogo, uwezi amini, amekataa ata kutaja jina lake” alisema Insp Aisha, huku anacheka kidogo, “ulishindwa kumlaghai ata kwa atabasamu?” anauliza ASP Ayoub Mzee, akionyesha kumlahumu Insp Aisha.

“nini kumlaghai, niliongea nae kwa moyo wa dhati kabisa, na yeye aliona, lakini wapi” alisema Aisha, huku anaachia kicheko chenye kijiaibu flani, lakini ASP Ayoub Mzee aonyeshi kuzingatia aibu ya Insp Aisha.

“jiandae, nazani utajibu maswali kama aya kwa RPC, maana aliamini kuwa tayari utakuwa, umesha fahamiana na yule dogo, anae tufarakanisha na Nyondo” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anashika kiuno kwa uchovu.

“haooo wanatoka” anasema Aisha, alikuwa anatazama kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo kuu, la makao makuu ya jeshi ili pendwa lwenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao.

ASP Ayoub Mzee ananza kutembea kuwa fwata viongozi wake, kule wanakotokea, Aisha nae anamfwata Ayoub Mzee, “nivigumu kuamini, kama TSA wanaweza kuvamia chuo cha uhalimu, na kusababisha ilo, au kuna mtu hatari alikuwa amejificha hapo chuoni” wakina Aisha walimsikia staff officer, akiuliza kwa sauti yenye mshangao na mashaka.

“inawezekana walipata habari za kipelelezi, kuwa kuna mtu hatari, asa huyo mwanamke alietoweka baada tu ya kufanya mauwaji” alijibu RCO Zamoyoni Mpeta, wakina Aisha wakiwa wamesha wakaribia, wakuu wao wakazi waliokuwa wanaelekea kwenye magari yao. . ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!