TOBO LA PANYA (68)

SEHEMU YA SITINI NA NANE

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA SABA: “inawezekana walipata habari za kipelelezi, kuwa kuna mtu hatari, asa huyo mwanamke alietoweka baada tu ya kufanya mauwaji” alijibu RCO Zamoyoni Mpeta, wakina Aisha wakiwa wamesha wakaribia, wakuu wao wakazi waliokuwa wanaelekea kwenye magari yao. . ….ENDELEA

“kwanini sasa muda wote, mauwaji yatokee eneo ilo ilo la chuo” aliuliza RPC kwa sauti yenye mashaka, huku wanasimama kwenye ubavu wa gari la RPC, “lazima kuna namna, au huyo mwanamke ni mshirika wa yule muuwaji?” alie tilia shaka ilo, ni staff officer.

“tuachane na hiyo” alisema RPC, kisha akawatazama wakina Aisha, “Ayoub Mzee na Insp Aisha” aliita RPC, kwa sauti ya kawaida, “afande” wanaitikia kwa pamoja, wakina Insp Aisha, huku virho vina wadunda, kwamaana awakujuwa wataambiwa nini baada ya hapo.

“sasa mmekabidhiwa lasmi, jukumu la kuhakikisha yule muuwaji anapatikana, kuhusu usafiri, mtatumia gari la kitengo cha CID, lenye namba za kiraia, mavazi muda wote mtatumia ya kiraia” alisema RPC, huku anawatazama wakina Insp Aisha kwa zamu.

“ndiyo afande” wanaitikia wakina Ayoub Mzee na Insp Aisha, ikiwa ni kukubaria jukumu walilopewa, “kwa upande wa silaha, mtakuwa na SMG pia mtakuwa chines pistor, ambazo mtakaa nazo mpaka mwisho wa jukumu, taarifa zitaenda moja kwa moja kwa RCO” anasema RPC, kwa sauti ambayo kikawaida aikuwa kali, lakini ilitoa maelekezo mazito.

“kazi inatakiwa ikamamilike haraka sana, vipi kuna lolote mnataka kushauri” alisema RPC huku anamtazama ASP Ayoub Mzee, “hapana afande, hapa ni kazi tu” ilo ndilo jibu la ASP Ayoub Mzee.

RPC anamtazama Insp Aisha Amary, “afande kwa ushauri wangu, ni kwamba, ilizoezi lisitumie nguvu wala silaha, nivyema kama tukitumia dipromasia” alisema Insp Aisha, na kuweka kituo kidogo.

“kwanini Insp, hivi unazani kuna muuwaji anae kamatwa kwa dipromasia?” aliuliza RPC, kwa sauti ya mshangao na hamaki, huku anamtazama Insp Aisha, ambae alionyesha uoga kidogo, lakini akajikaza.

“samahani afande, ukweli ni kwamba, yule kijana ni hatari sana, pengine ana mafunzo ya juu ya ujasusi, japo sina uhakika, maana anauwezo mkubwa sana wakupiga, kwa kutumia mikono na visu, sijajuwa kuhusu bunduki, ila ajiulizi mala mbili, anapopelaka kisu shingoni kw amtu” alifanunua Insp Aisha.

Hapo RPC, akawatazama viongozi wenzake, kama vile wanaulizana jambo, “au ni muuwaji wa kukodi, toka makundi ya kigaidi ya nje ya nchi, wanalipiza kisasi kwa Nyondo” anauliza staff officer, huku anawatazama wenzake.

“kama niivyo, basi amuue Nyondo haraka, siyo anatuletea mtafaluku” alisema RPC, kwa sauti ya hasira, akionyesha kuchoshwa na jambo lile, “lakini hatuwezi kuacha kumchunguza, na kumfahamu huyu mtu” alisema tena RPC.

“pia mkuu, sisi jukumu letu ni kumfwatilia huyu mtu, maana tayari anamaadui, zake ambao na sisi ni kama maadui zetu” alisema ASP Ayoub Mzee, “mpaka hapo nazani mme elewa, mnaweza kuendelea na kazi” alisema RPC, kisha akafungua mlango wa gari lake na kuingia ndani.

RCO na staff officer nao awakusubiri tena, maana wakati gari la RPC linaelekea kwenye geti, nao wakaingia kwenye magari yao, na kuondoka zao, wakiwaacha ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, wakiwasindikiza kwa macho.

“kifuatacho afande?” anauliza Insp Aisha, “sidhani kama kuna kingine zaidi ya mimi kumsubiri mama Farid na kupumzika kidogo, sijuwi kama watakumbuka kuni bebea japo pilau kidogo, maana nina njaa kali” alisema ASP Ayoub Mzee, na kumfanya Insp Aisha acheke kidogo.

“nitachukuwa askari wanipeleke nyumbani, nikachukue nguo za kubadiri, kisha nije nilale hapa hapa kituoni, yule mshenzi anaweza kuja kunichukuwa nyumbani” alisema Insp Aisha, huku anamtazama A-Insp mmoja, aliekuwa+ amekaa pamoja na kundi la askari, waliopo tayari kwa kazi ya doria siku ile. ****

Naaaaaaaaaam!, saa sita kasoro za usiku, mji wasongea ulionekana kupoa kwa upande wa katikati ya mji, na mitaa mingine ya pembezoni, lakini tofauti na mtaa wa mateka uhindini.

Nyumbani kwa bwana Nyondo, sauti za music wa taratibu wa maombolezo, ulikuwa unaendelea, watu walionekana wengi sana, upande wa nje wa uzio wa jengo ili.

Bado vijana walionekana kuangalia usalama eneo lote la uzio wa jengo ili kubwa sana, huku watu wakionekana kuto kuwa na mpango wa kuondoka usiku ule.

Watu walikuwa wakiongea na kucheka kwa pamoja, kama vile wapo kwenye sherehe, au tafrija flani, pia walionekana wanawake kwa wanaume, katika mikao ya kutongozana, au kuonyesha mahaba mazito.

Kwahakika ni ule music wa maombolezo toka kwenye speeker kubwa, ndio ambao, ungekujulisha kuwa, mahali hapa kunamsiba, vinginevyo ni kwamba, liha ya uwingi wawatu, lakini hakuna mtu alie onyesha kuguswa na msiba ule kwa uchungu.

Wakati huo huo, tunayaona magari manne, aina ya land rover diffender, yakitoka ndani ya uzio, kupitia kwenye lango la nyuma, lile ambalo waliingia wakati wanamleta Insp Aisha, hakuna alie weza kuwaona vijana wenye silaha waliokaa ndani ya magari yale, wakijigawa wanne kila gari.

Nayo yakashika uelekeo wa mjini, kwa mwendo wa kasi tena kasi ya ajabu, na kuacha maswali mengi, kwa watu waliokuwa wamekaa pale nje, “mjini hakunogi huku, wakikukuta hao umesha kuf” alisema mmoja wa watu aliekuwepo pale nje, ni kama walikuwa wanafahamu kituflani.

Huko ndani ya uzio mambo yalikuwa kama nje, japo huku ndani kwa heshima kidogo, maana ata watu waliokuwa huku ndani, ni watu wenye heshima zao, ata bwana Nyondo nae alikuwepo eneo lile la ndani, amejituliza kwenye kiti chake, huku Kichondo akiwa amesimama nyuma yake.

“Kichondo, hivi huyu Manda amesha ondoka kweli?” anauliza Nyondo, kwa sauti kavu, iliyojawa na hamu ya kupata taarifa za mafanikio, “wamesha toka boss, nimesikia magari yakiondoka” anajibu Kichondo.

Upande wa nje, linasimama gari dogo aina ya Toyota mark 2, kisha anashuka mwanamke moja mtu mzima, alie jitanda vitenge kadhaa, akifunika nywele zake vizuri, ata uso wake ulionekana kidogo sana. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!