TOBO LA PANYA (69)

SEHEMU YA SITINI NA TISA

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NANE: Upande wa nje, linasimama gari dogo aina ya Toyota mark 2, kisha anashuka mwanamke moja mtu mzima, alie jitanda vitenge kadhaa, akifunika nywele zake vizuri, ata uso wake ulionekana kidogo sana. ….ENDELEA

Anaingia ndani ya jengo uzio ule akiwapita walinzi wawili, ambao mida hii walikuwa wanakagua kwa macho, mwonekano wako ndio unakuhukumu, na uzri ni kwamba, walikuwa wanatazama sana vijana wakiume.

Mwanamke mtu mzima, anapitiliza moja kwa moja upande waliopo wanaume, na kuanza kuwa salimia moja baada ya mwingine, huku akiwapa pole, kuelekea upande aliopo bwana Nyondo.

Kichondo na Nyondo wanaendelea na maongezi, “sijuwi nitamfanya nini yule mtoto, nina hakika nitamzika mzima, ndani ya kaburi la Lukas” alisema Nyondo kwa sauti ya chini, huku hasirakali ikiwa inaonekana usoni mwake.

“naamini wakina Manda watakuja nae…” Kichondo akuweza kumaliza alichokuwa anaongea, maana tayari kuna mwanamke mtu mzima alikuwa amesha wafikia, “kaka pole na msiba” alisema yule mwanamke, kwa sauti iliyopoa, huku anampa mkono Nyondo.

Nyondo nae ampatia mkono, “asante sana kazi ya mungu aina makosa” alisema Nyondo, kwasauti tulivu yenye kiwango cha mstaarabu flani, mfano wa kuigwa, mungu awatie nguvu” alisema yule mwanamke, huku anaachiana mikono na Nyondo.

“pole mwanangu, kwa kumpoteza rafiki yako” anasema yule mama mtu mzima, huku anampatia mkono Kichondo, nae anaupokea “asante mama, pole na wewe” anasema Kichondo, huku wanaachiana mikono, “asante mwanangu, mungu afanye wepesi katika kipindi iki kigumu” alisema yule mama kisha akaanza kuondoka zake, akielekea upande waliko wanawake, huku Kichondo na Nyondo wakimsindikiza kwa macho.

Mama mtu mzima, anapo wafikia wakina mama wenzake, anaanza kuwasalimia, mmoja baada ya mwingine, kama alivyo fanya upande wa wanaume, “sidhani kama namfahamu huyu mwanamke” alisema Nyondo, huku wanaendelea kumtazama yule mama.

“nimejaribu kumtazama pia, lakini sijaweza kumfahamu, wanatufahamu wengi, kuliko tunao wafahamu” alisema Kichondo, huku bado wanaendelea kumtazama yule mwanamke, ambae alisalimiana na baadhi ya wanawake, kisha akaelekea getini na kutoka nje, akitokomea gizani.***

Naaaaaaaaam!, pembezoni kabisa mwa mtaa wa seed farm B, upande wa kaskazini, giza lime tawara, kotokana na kukosekana kwa umeme katika eneo ili, BMW jeusi linasimama nje ya kibanda cha udongo, kilicho jengwa pembezoni kabisa mwa kichuguu, kisha taa za gari zina zimwa, ikifwatiwa na engine.

Unapita muda mrefu, bila mtu kushuka, kama ungekuwa unasubiri jambo ilo, basi ungehisi kuwa, dereva amepitiwa na usingizi ndani ya gari, maana zilipita dakika tano nzima.

Ndipo anashuka Hance anashuka toka kwenye gari, kisha anatazama kushoto na kulia kabla ajafunga mlango wa gari, nikama bado ajalizika, anatazama kwenye mlango wa banda la udongo, kabla ajatazama chini ya mlango, nikama ajaona kitu chochote.

Lakini basi, ile anatazama kwenye sakafu ya dunia, yani chini, karibu na mlango, akaona kitu flani, haraka sana akapeleka mkono wake ndani ya koti, eneo la kifuani, na kuibuka na kisu.

“SA-54” anaita Hance kwa sauti ya wazi, ni mala baada ya kuona alama ya mchoro flani, iliyochorwa kwa kijiti au udongo, ikiandikwa 5F4, “mh!, kumbe bado wa moto” inasikika sauti ya kike toka nyuma ya gari.

Hance anageuka na kutazama upande ambao sauti imetokea, anamwona mwanamke mkubwa kidogo kwake, alie beba begi dogo mgongoni, na kitabu mkononi, “Farida, una hakika hakuna alie kufwata mpaka hapa?” aliuliza Hance kwa sauti ya upole, na utulivu.

“nipo mwenyewe, wala usiwe na wasi wasi” anasema Farida, kwa sauti ambayo aikuwa na mshaka yoyote, “usiniambie kuna ujumbe umeniletea wakati unauwezo wa kupiga simu kwa Kingumwile” alisema Hance kwa sauti yenye mashaka.

“hapana Panya sina ujumbe wowote, ila nimesha dondosha SA mmoja huko chuoni, sasa natafutwa na TSA” alieleza Farida, na kumfanya Hance atulie kidogo, akishusha pumzi ya uafadhari.

“ilikuwaje wakagundua uwepo wako?” anauliza Hance ambae sasa anaegemea gari lake, “nazani kuna watu walikuwa wanamfwatilia Nancy, waliona wakati namleta barabarani” alisema Farida, ambae bado alikuwa ameshikilia kitabu chake, huku amebeba begi lake dogo mgongoni.

“ok!, hatutakiwi kupoteza muda” alisema Hance, huku anageuka na kufungua mlango wa gari, “nenda kapumzike nyumbani kwa wazazi wangukule mabatini, hakikisha wanakuwa salama” anasema Hance huku chomeka funguo kwenye tundu la switch, na kuliwasha gari.

“sasa nafutwa na makundi matatu tofauti, polisi, TSA na hao wapuuzi wasio zionea huruma shingo zao ” alisema Hance, huku anapisha mlango kwa maana ya kumluhusu Farida aingie garini, “hivyo basi naomba uwe mlinzi wa gongo wangu” alisema Hance, muda wote Farida anamsikiliza.

“aina shida, nitakuwa macho muda wote” alisema Farida huku anaingia kwenye gari, anashusha kioo cha gari, huku anafunga mlango, “usipoteze muda, unaweza kwenda” alisema Hance, na hapo Farida akakanyaga mafuta, na gari likaondoka kuelekea upande wa mjini.***

Upande wamashariki, mwa mji wa Songea, nako kumepoa kama mitaa mingine, ya mji huu, kwenye barabara iendayo mikoa ya kusini, maeneo ya mahenge, tunaliona Nissan patrol, lina tembea taratibu kuelekea mashariki zaidi.

Ndani ya gari kuna watu watano, yani baba na mama Eric, Eric mwenyewe na mschana Eveline, wengi umwita muzungu, kutokana na rangi yake ya ngozi, iliyo egemea kwa upende wa baba yake ambae ni mjerumani, pia alikuwepo mschana mdogo Vestina, maongezi yalikuwa mengi sana ndani ya gari, mama Eric akiongoza maongezi hayo.

Lakini ilikuwa tofauti kidogo, maana licha ya maongezi kubwa mengi na sauti ya juu, kuliko redio ya kwenye gari, lakini mzee Haule alikuwa kimya kabisa, anaendesha gari huku macho ameyaelekeza mbele.

“ila yule mama alipokea kichapo kitakatifu” alisema mama Eric, akisimulia hadithi ya mama yake wakambo Amina, miezi michache iliyopita, “mwisho ameolewa na mganga” alisema Eva, ambae ambae uzuri na mwonekano wake, umeelezewa kwenye hadithi na simulizi ya (#MWALIMU_NAE_ANATAKA).

Utulivu wa mzee Haule, aukuwa bure, hakika muda wote mzee Haule, alikuwa anajaribu kuwaza na kufukiri jambo, “hivi nimepeleka wapi uwezo wangu wa kung’amua mambo?” anajiuliza mzee Haule, kimoyo moyo, akuonyesha kujilahumu.

Gari linaenda, wakazidi kusogea mbele, sasa wanakatiza mitaa ya kituo cha polisi, kinacho kaliwa na kikundi maalumu, cha FFU, ambacho kipo mita chache toka njia panda ya Songea boyz.

“siku za nyuma nimegundua mambo mengi, na kuyafanikisha, inakuwaje huyu mtoto mdogo, SA-26, ambae anauwa maeneo ya huku huku nyumbani….” anajisemaa mzee Haule, ambae anasita ghafla, huku anatazama upande wake wa kulia, yani nje ya barabara, ambako anaona picha flani iliyo jirudia kichwani mwake, baada ya kuiona msaa kadhaa yaliyopita. . ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!