
SEHEMU YA SABINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NNE: Lakini basi, wakati mzee Haule na bwana Mahundi wakiwa wanawatazama wale jamaa waliokuwa wanabadiri magazan za silaha zao, kwakutumia darubini zenye uwezo wakuona gizani, mala ghafla wanaona tukio la kushangaza, “mungu wangu, nini kile” anauliza mzee Haule huku anatoa darubin machoni mwake, na kumtazama Mahundi, ambae pia alikuwa amefanya vivyo hivyo. ….ENDELEA…..
Kwamaana waliona tukio la kushangaza sana, kwamba kitu kama kimvuri kilipita kwa haraka, karibu ya mmoja kati ya vijana wale, fumba na kumbua kicha cha yule jamaa kikaonekana hewani kikiambaa mbaa, kama kishada na kutwa chini kama mpira wa volley ball ulio pigwa na mpigaji yani spaiker.
Wote wawili wanasogeza darubini zao machoni, nakutazama upande wa tukio, ambako wanawaona wale jamaa, wakielekeza bunduki zao, kwa mtu yule ambae sasa anaonekana vizuri, akiwa na bukta ndogo, bila shati wala viatu mwilini mwake.
Lakini kijana huyu mwepesi kama karatasi, anapita karibu ya jamaa mwingine ambae alikuwa anajiandaa kuinua bunduki, ili kumshambulia jamaa huyu mwenye kibukta.
Bahati aikuwa yake, maana sekunde aikutosha, tayari mkono wa kulia ulikuwa chini, huku umeshikilia bunduki, ukelele wa maumivu ulisikika kidogo sana, kabla kichwa cha mtu huyo kuonekana hewani, kikiwa kimesha tenganishwa na kiwili wili.
“Mahundi unaona, niyeye mwenyewe, ni hatari sana huyu mtoto, lazima tungepoteza SA wengi sana, na tusinge mpata” alisema mzee Haule, kwa sauti ya kunong’ona.
“nikweli kabisa kaka, ebu ona…” alisema Mahundi, huku wanashuhudia wale vijana wakitawanyika na kuanza kukimbia, kuelekea kwenye gari, huku wanapiga risasi hovyo, wakati huo, mtu wanae mhisi ni SA- 26 akuonekana tena.
Jamaa wanaingia kwenye gari na kuondoka mbio mbio, kueleka upande wa mjini, wakiwa wameacha miili ya wenzao wawili, pamoja bunduki zao, wakapita palewalipo jificha wakina mzee Haule.
“mh!, kaka, huyu dogo ni hatari, siyo wa kumwingia kichwa kichwa, wacha kesho nitajuwa la kufanya” alisema mzee Haule, huku anainuka kwa tahadhari, na kujitoa kichakani, akifwatiwa na bwana Mahundi.
“kaka naamini katika mipango yako, lakini kuhusu huyu jamaa naomba uwe makini sana” alisema Mahundi, ambae nikama aliingiwa na wasi wasi, “imekuwa vyema wale wapuuzi wamejiingiza kwenye chambo, tumejionea wenyewe” alisema mzee Haule, huku wanaendelea kutembea kuelekea kusini walikotokea.****
Meter elfu tatu, toka kwenye shimo la Panya, upande wa kusini, magari mawili ya polisi, yenye askari sita kila gari, wenye bunduki na mikebe kadhaa ya risasi, huku seat za mbele za kukiwa na dereva pamoja na afisa mkuu.
Gari la mbele likiwa na ASP Ayoub Mzee, gari lanyuma likiwa na Insp Aisha Amary, “hallow farasi namba moja, toka farasi namba mbili, pokea ujumbe over” ilisikika sauti toka kwenye redio, ya mmoja wa askari aliekuwa nyuma ya gari la mbele.
Sauti hiyo inasikika pia kwenye redio za maafisa awa wawili waliokuwa wamekaa seat za mbele, yani Ayoub Mzee na Insp Aisha, “farasi wa pili tuma ujumbe, over” inasikika kwenye redio zote, huku magari yaliyokuwa ya akatiza seed farm A, kuelekea chuo cha ualimu.
Wote wanatega sikio kwa umakini mkubwa, “toka farasi wa pili, upande wa kaskazini, kumesikika mlio wa njugu zinakaangwa, julisha kama na wewe umesikia over” ndivyo ilivyosikika sauti ya redio, ikipokea ujumbe toka gari la nyuma, ambalo alikuwepo Insp Aisha.
“toka farasi wa kwanza, imesikika iyo milio, lakini atukuwa na uhakika ni upande gani, over” alijibu askari wa gari la kwanza, “toka farasi wa pili, julisha kwa Papa Chale ili tuelekee upande huo, roja sofa over” alisema askari wa gari la pili.
Hapo kabla ata yule askari ajasema lolote kwa ASP Ayoub Mzee, tayari yeye mwenyewe alisha toa maelekezo, “dereva geuza gari, kuelekea seed farm B” alisema ASP Ayoub Mzee, nakama vile dereva alisha fahamu kinacho fwata, maana ghafla dereva alipunguza mwendo kidogo, na kugeuza gari kwa mtindo wa U turn, akifwatiwa na mwenzake wa gari la nyuma, safari ya seed farm B, ikaanza mala moja.
Msafara unaenda mpaka njia panda, ambako msafara unakata kona kulia, na kufwata barabara endayo Tunduru, magari yote mawili yanaongeza mwendo, na kukatiza kwenye barabara ya vumbi (wakati huo), mpaka magari hayo yanapo ikuta kona ya makazi ya chama tawara, (kwasasa amsha popo).
Magari yanapunguza mwendo, na kukata kona kushoto, kwa kufwata, huku mbele yao wakishuhudia magari mawili aina ya land rover defender, yakisha kwa speed kutokea kaskazini, mwa mtaa huu wa seed farm B, ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU