
SEHEMU YA SABINI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO: Magari yanapunguza mwendo, na kukata kona kushoto, kwa kufwata, huku mbele yao wakishuhudia magari mawili aina ya land rover defender, yakisha kwa speed kutokea kaskazini, mwa mtaa huu wa seed farm B, ….ENDELEA…..
Fumba na kufumbua, tayari magari yale yalisha katiza ubavuni mwao, nayo yanaingia barabara kuu, na kutokomea upande wa mjini, wakiwaacha wakina Ayoub Mzee, wanakosa maamuzi.
“nani wale, kwanini ufwati?” anauliza Ayoub Mzee, huku anageuka kutazama nyuma, ambako yale magari yalikuwa yamesha toweka, yakiacha ishara ya taa nyekundu za nyuma.
“afande, kwa ufinyu wa barabara, lazima tukageukie pale mbele” alijibu dereva wa gari la mbele, huku anaongeza mwendo, kuwai sehemu ya kugeuzia, “achana nao kwa hapo atuwezi kuwa kuta, nivyema kama tutaelekea mbele, tukatafute eneo la tukio” alisema ASP Ayoub Mzee.
Hapo madereva wanalanyaga mafuta kueleka kaskazini zaidi, huku wanajiuliza wale jamaa wenye yale magari ni wakina nani.***
Wakati huo huo, mzee Haule na vijana wake, wapo mita chache, upande wandani toka kwenye nyumba yake, amesimama mbele ya vijana wake wa TSA, anaongea mawili machache.
“nazani kila mmoja amesikia na kujionea, kazi ya SA- 26, hivyo basi naomba wote kwa pamoja, tukubariane kuwa, SA-26, nizaidi ya KM” aliongea mzee Haule akimaanisha kuwa ni zaidi ya killing Machine.
“kwamaana hiyo basi, kumkamata SA- 26, inaitaji busara na mbivu zaidi, siyo bunduki na visu, je kuna mwenye wazo au ushauri?” aliongea mzee Haule, na ndipo mmoja kati ya wale vijana wake alipo nyoosha mkono,kuomba kutoa maoni yake.
“sema kijana, una maoni gani” alisema mzee Haule, akimtazama yule alie nyoosha mkono, “mkulugenzi, mimi nataka kujuwa kwanini TSA wanahisi SA- 26 nimsaliti, kwanini wasongee nae na kumtumia kama reserve, maana ni mtu mwenye uwezo mkubwa na anafaa kwa majukumu magumu” alisma yule kijana.
Hapo mzee Haule anatulia kidogo, anawaza sababu ya TSA kutaka kumuuwa SA-26, nikwamba anaweza kutumiwa na maadui wa taifa, kuuwa viongozi, au kuhujumu taifa.
Lakini hizi ni hisia tu, ila bado anaweza kushauri, “ni swala gumu kidogo, nitaongea na uongozi, ili nione kama, wanaweza kuchukuwa wazo ilo au la” alijibu bwana Haule, “vipi kuna mwingine mwenye wazo, kabla sija waluhusu mka pumzike?” anauliza tena mzee Haule.
Mwingine ananyosha mkono, “ok! sema kijana” anasema mzee Haule, na yule SA anaanza kutoa maoni yake, “mlugenzi mimi shauri jambo moja, kama huyu SA-26 hakufanya kosa lolote, basi TSA iingie nae mkataba mzuri, au kuwa mwalimu wa karate, au kupangia jukumu lolote la kiserikali, nje ya TSA” ayo ndiyo maoni ya kijana huyu.
Mzee Haule anatabasamu kidogo, “mawazo mazuri, yote nayafanyia kazi” alisema mzee Haule ambae ghafla alishtuka na kutazama upande wabarabarani, ambako palionekana magari mawili ya jeshi la polisi yakielekea upande wa kaskazini, yani kule nyum,bani kwa SA – 26, huku yakiwa yame jaa askari kwenye kibebeo chake.
“kumekucha, hao nao sijuwi wanalekea wapi” anasema mzee Mahundi, na wote wanacheka kidogo, kabla ya kuagana, na mzee Haule kiingia ndani ya nyuma yake, huku TSA wakiingia kwenye magari na kuondoka zao, kuelekea mjini.***
Yap!, mwana dada Anastansia, ambae dakika `nyingi zilizo pita, alishuhudia tukio lote, kupitia computer ile ya ajabu, anatoa macho kwa mshangao, akikodolea macho kioo kile cha computer, ambayo sasa alikuwa anaonekana kijana mpole, aliekuwa anakokota miili ya wanadamu wawili waliokosa vichwa, kupeleka kichakani.
Anastansia anamwona kijana huyu hatari, mwenye maamuzi ya haraka na uwezo wa hali ya juu, katika kutekeleza mauwaji, anatokomea na miili ile, kwenye vichaka.
kisha anaibuka tena, na kuingia kwenye banda la udongo, ambalo limejaa giza, ila akaisana, maana sekunde chache anaibuka akiwa na sururu na chepe mkononi mwake, anaanza kufukia damu pale chini akitumia chepe yani sped, huku anaokota baadhi ya maganda ya risasi.
Anapo lizika na usafi alioufanya, kijana anatokomea tena kichakani, akiwa na vifaa vyake, Anastansia ambae picha ya tukio la uchinjaji alilotoka kulifanya kijana huyu mpole, dakika chache zilizopita.****
Naaaam!, kilomita moja na nusu toka kwenye nyumba ya kijana Hance au Panya, yani SA- 26, yani shimo la Panya, kama yeye anavyo liita, tuna yaona magari mawili ya TSA, yakitembea kwa kasi kuelekea upande wa barabara kuu ya mikoa ya kusini.
Mita chache mbele yao wanayaona magari mawili ya polisi, yakipita kwa kasi kuelekea upande wa kusini, kule ambako wao wametokea nusu saa iliyopita, yani kwa wakara mwenyezao wanae mtafuta, huyo ni SA- 26. , ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU