
SEHEMU YA SABINI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA SITA: Mita chache mbele yao wanayaona magari mawili ya polisi, yakipita kwa kasi kuelekea upande wa kusini, kule ambako wao wametokea nusu saa iliyopita, yani kwa wakara mwenyezao wanae mtafuta, huyo ni SA- 26. , ….ENDELEA…..
“wanaenda wapi hao nao, waache wakamchokoze yule kichaa, akate shingo zao” anasema bwana Mahundi, huku yeye na dereva wake wakicheka kwa dharau, “kwa habari za huyu jamaa, anaonekana ni hatari sana” anasema dereva, huku anaendelea kuendesha gari, kuelekea barabara kuu.
“ukimwona uwezi amini kama ni yeye, labda ukutane nae kwenye matukio yake” alisema bwana Mahundi, kwa sauti ambayo ilielezea kile alicho kiongea, “kwanza yupoje huyo mtu?” anauliza dereva kwa sauti yenye shahuku ya kutaka kumfahamu, “aeleweki” ilo ndilo jibu la Mahundi.***
Naaaaam kwenye shimo la Panya, bado Anastansia anatazama kioo cha chaile computer ya ajabu, tayari dakika ishirini zimesha pita, kijana mpole ajatokea toka kichakani,
Anastansia moyoni mwake anajikuta anaingiwa na wasi wasi na hofu, “mh!, sasa wakimkamata kule kichakani itakuwaje” anawazaanastansia akionyesha kumwonea huruma kijanahuyu, asie mfahamu kwa majina.
“atakama anawapiga, lakini wanaweza kumzidi ujanja” anawaza Nancy, ambae moyoni mwake anahisi kuwa maisha bila kijana huyu ayawezekani, sijuwi ni kwanini, labda kwaajili ya usalama wake Anastansia.
“hivi itakuwaje kama tulala wote kitandani?” anajiuliza Anastansia, huku anatazama kitanda, “kitanda kikubwa, lakini sijawai kulala na mwanaume kitanda kimoja” anasema Anastansia huku aanchia tabasamu, na kurudisha macho kwenye computer.
Hapo Anastansia ambae sasa anahisi mkojo umembana, anamwona kijana mpole, akiwa anaibuka toka kichakani, akiwa na vifaa vyake, “yes, huyooo anakuja” anasema Nancy huku anaachia tabasamu pana, na kutazama kitanda, sijuwi itakuwaje leo” alisema Anastansia, huku anarudisha macho kwenye kioo cha computer.
Lakini ile anarudisha macho kwenye computer, amwoni tena kijana mpole, ni kama ametoweka, na kutokweka kwake nikama amerudi kichakani, tena kwa haraka, maana asingeweza kufikia tobo la Panya, kwa uharaka wa kiasi kile.
Kabla Anastansia ajajiuliza nini kimetokea, mala anayaona magari mawili ya polisi, yanasimama mbele ya kibanda cha udongo, ambacho ndio mlango wakuingilia shimoni,.
Anastansia anawaona polisi wachache, wote wakiwa na alama za vyeo maegani mwao, wawili waliwa waevalia nguo nadhifu za kiraia, mmoja wapoa akiwa wakike, wanashuka toka kwenye gari, na kujikusanya pamoja.
“mh!, yani adi polisi wamesha juwa tupo hapa” anajisemea Anastansia, huku endelea kuwatazama wale polisi, ambao sasa wanaonekana wakiongea, mawili matatu, kama vile wanajadiri jambo na kuelekezana, maana walikuwa wanaonyeshana eneo la mbele zaidi.
Japo Anastansia alikuwa amebanwa na mkojo, lakini akuwa tayari kuacha kuwatazama wale polisi, ilikuwajuwa kama ujio wao, ni kwamba wamesha ng’amua uwepo wa tobo la Panya au la.***
Naaaaaaaam!, sasa turudi mateka uhindini, moja kwa moja tuna zungumzia nyumbani kwa bwana Augustino Nyondo, ambako watu ni wengi kwa idadi ile ile ya mwanzo, kwamaana awaja ongezeka, ila walizidi kuchangamka, kutokana na vilevi na vivuto walivyo kuwa wanavitumia.
Upande wanje wa walijaa vijana wakike na wakiume, ambao walionekanawakiwa wamesimama kwa makundi, wapo waliokuwa wanakunywa pombe toka kwenye grocer ya jirani, wapo waliokuwa wanakunywa pombe za kienyeji, zile za vimea, na zile msimu kama vile ulanzi, na nyinginezo.
Pia wapo waliokuwa pembeni kabisa, wakivuta bangi, na wengine wakipeana mapenzi moto moto, na wapenzi wao wakike, ambao walionyesha wazi kuwa, muda wowote, wanaweza kuingia gizani na kupeana dudu.
Wakati tuangazia hali iliyopo nje, mala tunayaona magari mawili aina ya land rover defender, yakipita kwa speed na kwenda uingia kwenye geti la nyuma, yakichukuwa umakini wa watu waliokuwepo pale nje, ambao walitoa macho kwa mshangao.
Upande wa ndani ya uzio, wanaonekana watu wengi, wenye mwonekanani wa VIP, wakiwa wamekaa kwenye viti vyao, baada yao wakiwa na vinywaji, vyenye vilevi, yani pombe.
Safari hii ilikuwa tofauti kidogo, kwamaana utulivu wa wakati ule ulipungua kidogo, na sasa maongezi yalipamba moto, na watu walionekana wamechangamka sana, tofauti na ilivyo kuwa masaa kadhaa yaliyopita, iwe upande wa wanaume au wanawake.
Eneo lile lile la ndani, upande wa wanaume tuna mwona bwana Nyondo, alie kaa kwa kujitenga kidogo, akuwa peke yake, alikuwa pamoja na mlinzi wake wakaribu na kijana nae muamini, yani Kichondo, kijana ambae siyo tu kuwa mwenye mwili mkubwa, ulio jengeka kimazoezi, pia alikuwa na katiri kweli kweli, maamuzi mengi, ya mauwaji ambayo Nyondo anayatoa, mtekelezaji ni Kichondo.
“kwahiyo huyu mpuuzi wanamfahamu, na wanashindwa kumkamata, alafu wananitisha, eti hooo!, ni mtu hatari” anaaema Tino Nyondo, “wameamua kuleta dharau, sababu atujawafanyia tukio” alisema Kichondo, na wakati huo huo wanamwona Manda, yule kijana ambae anaongoza kundi ili la mwisho.
Anasogea mpaka alipo wafikia wakina Nyondo, “samahani boss, tumerudi mikono mitupu, yule jamaa ni hatari, tunaitaji kujipanga vizuri” alisema Manda, ambae uso wake unaonekana wazi kuingiwa na mshtukio, kwa ile alicho kiona, kule kwenye shimo la Panya.
Nyondo anageuka ghafla, na kumtazama Manda kwa macho makali yenye hasira, anataka kusema kitu, lakini anajizuwia, anatazama upande wake wa kushoto, ambako wanaonekana waombolezaji wakiwa wanamtazama.
Anaachia tabasamu kidogo, kisha anamtazama Manda, “sitaki kusikia makosa tena, nataka kuona huyo mjinga umnaleta kwangu, Lukas azikwi peke yake, atazikwa na huyo mshenzi” alisema Tino Nyondo, kwa sauti ya chini, yenye hasira, akimaliza na ishala ya mkono kwamba aondoke.****
Yaaaaap!, Insp Aisha, ASP Ayoub Mzee na askari wengine wawili, bado walikuwa wamesimama, mbele ya banda la udongo, wanajadiri jambo, “huko mbele sizani kama kuna eneo la makazi ya watu” alisema ASP Ayoub Mzee, akionyesha upande wa kaskazini.
“ila tungejaribu kusogea huko chini kidogo, tunaweza kuona kitu kinachoweza kutusaidia kujuwa kilichotokea” alisema Insp Aisha Amary, “mh!, lakini afande, huko ni bondeni, kama tukio lingetokea huko, sauti isingefika fika mbali, huko tuna jisumbua bule” alisema askari mmoja, akionyesha kuto kukubariana na wazo la Insp Aisha. , ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU