
SEHEMU YA THEMANINI
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TISA: Licha ya kuwa alikuwa bado amefumba macho, lakini mala kwa mala alionekana akitabasamu, sijuwi ilikuwa ndotoni, au alikuwa amesha amka, ila zingatia tabasamu lililokuwa linachanua usoni mwake, huku amefumba macho, na kujigeuza kila baada ya sekunde chache, yani mala alale chali, mala kiubavu, mala kifudi fudi. ….ENDELEA…..
Kabla ujajiuliza Hance yupo wapi, tunamwona akiwa nje ya kibanda cha udongo, kilichojengwa pembezoni mwa kichuguu kikubwa, akifanya usafi wa mazingira, yanayo zunguka kibanda cha udongo, lililo tobolewa na risasi, kuku wakionekana wanazunguka maeneo yale.
Hance alie kuwa amevalia kaptula chakavu ya jinsi, na tishert la kukata mikono, alikuwa ameshika fagio, anaondoa manyonya ya kuku, na baadhi ya kuku walio kuwa wamekufa, nadhani ni kwa kupiga risasi, kama wanavyoonekana mbuzi wawili, walio lala ndani ya banda lao, huku mwingine akiwa na jelaha kubwa pajani.
Wakati anaendelea kufanya usafi, huku anaokota baadhi ya maganda ya risasi, na vichwa vyeke, ambavyo jana alivisahau, huku kichwani mwake kijana huyu, alikuwa anawaza na kuvuta kumbu, juu ya tukio la jana usiku, siyo kuhusu mapigano na watu alio wauwa, au watu wanao mtafuta, wakiwepo TSA, ambao ni shirika lake la zamani.
Hiyo aikuwa shida kwake, kwamaana alisha zowea kufanya hivyo na amesha uwa watu wengi sana, tena kikatili zaidi, yeye alikuwa anawaza kuhusu jambo geni na tamu alilolifanya, na mschana mrembo na mzuri Anastansia, ambae siyo mzuri wa sura na mwili, ila pia alikuwa mtamu, kama biriani la siku kuu.
Wakati Hance akiwa anendelea kufanya usafi, mala akasikia michato ya vishindo, vya mtu aliekuwa anakimbia, kuja upande wake, kwamaana ya uelekeo wa barabara afifu.
Hance anageuka na kutazama upande huo, anawaona watu wawili, yani mzee mmoja wa makamo, na kijana mdogo, mwenye umri wa kati ya miaka 19na ishilini, wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya michezo, yani truck suit na raba, wanakimbia taratibu kuja upande ule.
Inamshangaza kidogo kijana wetu, maana ukiachilia kukosekana kwa utamaduni huu, hapa mkoani, yani wakufanya mazezi binafsi, ila pia alihisi jambo tofauti, kwa watu awa ambao anawafahamu, kuwa ni mzee Haule, na kijana wake, Eric, mchezaji mzuri wa mpira wakikapu.
Lakini Hance anaondoa mashaka, anasimama na kuwatazama kwa lengo la kutaka kuwasalimia, maana tayari walikuwa wamesha karibia usawa wa kibanda chake, kusalimia ni moja ya utamaduni wake, siyo kama kificho au danganya toto, ila ni toka akiwa mdogo.
Lakini wanapofika usawa waka makazi yake, Hance namwona mzee Haule anamweleza jambo kijana wake, “ngoja kwanza tusalimia, kijana mfugaji, unajambo la kujifunza kwake” ndivyo alivyo sema mzee Haule, kabla awajachepuka toka barabarani, na kuelekea pale alipo kuwepo, huku wanamtazama.
Wawili awa walikuwa katika hali tofauti kidogo, maana wakati mzee Haule alikuwa anamtazama Hance kwa macho yenye tabasamu la urafiki, huku kijana Eric, alikuwa katika hali ya hasira na chukizo, hii ni tangu anakuja toka mbali.
“bari yako kijana” alisalimia mzee Haule, huku wanasimama, mbele ya banda la udongo, “salama mzee shikamoo” aliitikia kijana Hance, kwa sauti yake tulivu, huku anaonyesha uchangamfu kidogo.
“Hance mambo vipi?” alisamia Eric, mtoto wa mzee Haule, akionyesha anamfahamu kijana huyu mpole, “poa tu Eric, naona unapasha kidogo” anasema Hance kwa sauti changamfu kidogo.
“dah!, mzee kanikulupua tu, wala siku panga kufanya mazezi” alisema Eric, akionyesha wazi kuwa akupenda kufanya mazoezi, asubuhi ya jumamosi ile, “kumbe nyie wawili mnafahamiana” anasema mzee Haule, kwa sauti yenye mshangao kidogo, na tabasamu la mafanikio.
“ndiyo mzee, namfahamu Eric, anacheza sana baskert ball, uwa naendaga kutazama mazoezi” alisema Hance, kwa sauti ya uchangamfu, huku anamtazama mzee Haule ambae alikuwa anatazama kile kibanda, kama ungemtazama bila kuzingatia, usingeona umakini alio tumia, ila Hance aliona vyema umakini wa mzee Haule alivyokuwa anatazama lile banda la udongo, na mazingira kwa ujumla.
“ok!, nivyema vyema mkifahamiana, ukizingatia kuwa, mnakaa mtaa mmoja” alisema mzee Haule, huku anatikisa kichwa kukubari, yani juu chini, “tuna onana sana, japo jamaa anaga story na mtu” alisema Eric, ambae sasa alianza kubadirika kidogo, na kuweka sura ya uchangamfu.
Wote wanacheka kidogo, kabla mzee Haule ajamtazama kijana Hance, “pole sana kijana, mifugo imepatwa na nini?” anasema mzee Haule huku wote wanatazama mbuzi na kuku waliokufa.
“nahisi kuna mdudu aliwavamia usiku, naitaji kuwa fukia” alisema Hance, ambae bado mkononi mwake alikuwa ameshikilia fagio, “dah!, hii ni hasara kubwa sana, inabidi ujenge banda zuri, maana huyo atakuwa nyoka tu” alisema Eric, akionyesha masikitiko yake.
Mzee Haule anamtazama Eric, “kanisubiri hapo pale, naitaji kuongea kidogo, na kijana mfugaji” alisema mzee Haule, na bila kuuliza Eric akatembea kurudi upande wa barabarani. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU