TOBO LA PANYA (84)

SEHEMU YA THEMANINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TATU: Lakini basi, kabla ata kundi alijaanza kuingia kwenye magari, mala akatokea kijana mdogo wa kiume, “baba, baba kunamtu anataka kuongea na wewe, anasema ni muhimu sana, kwaajili ya kumpata mtu unae mtafuta” alisema kijana yule mdogo, ambae kwa ufafanuzi, ni mtoto wa bwana Nyondo. ….ENDELEA…..

Kusikia hivyo bwana Nyondo akusubiri ata sekunde ipite, maana alitoka haraka na kuelekea ndani ya nyumba yake, huku akifwatiwa na Kichondo, huku wote wakiwa na shahuku, ya kujuwa huyo mtu anapatikana vipi, waende kumdabua haraka, maana leo walijivunia kwa uwingi wa watu na silaha, walizonazo.

Haraka sana, bwana Tino Nyondo, anaingia ndani ya nyumba yake akiwa ameongozana na Kichondo, moja kwa moja anaelekea kwenye meza yenye simu, ambayo mkonga wake ulikuwa pembeni.

Nyondo anaunyakuwa mkonga wasimu, na kukuuweka sikioni, “eleza haraka huyo mpuuzi yupo wapi” alisema Nyondo kwa sauti ya chini, lakini yenye ukali na hasira.

Kwanza kabisa anakutana na mguno wa kicheko, kifupi sana, Tino Nyondo anazidisha hasira, “ni wewe mpuuzi, ebu sema haraka upo wapi” anasema Tino Nyondo kwa sauti yenye hasira, huku akishindwa kuizuwia isipayuke, kamaana bila sauti za music huko nje, basi watu wangesikia wazi wazi.

“usiwe na haraka bwana Nyondo, najuwa una nitafuta, na una hasira na mimi, pasipo kuifikilia ujinga wako na wa mdogo wako, leo nataka tunamalizane” ilisikika sauti tulivu ya upole, isyo na wasi wasi ata kidogo.

“we mpuuzi, acha kumsema mdogo wangu, ambae umemuuwa kwa mikono yako, hakika nitakuzika mzima mzima, ndani ya kaburi atakalo zikiwa Lukas, kisha na fwatia familia yako, sema haraka hupo wapi” alisema Nyondo kwa sauti ya chini, tena, safari hii ikiwa na hasira kuu, hasira ambayo ilibakia kidogo abamize mkonga wa simu.

Kinapita kimya kifupi, “we mpuuzi hivi unasikia kweli, nauliza hupo wapi tuje kumalizana” anasema mzee Nyondo kwa sauti ya juu ya ukali, yenye hasira, ambayo ilikuwa inapanda kila dakika.

“nakushauri usiharakie kukutana na mimi, maana leo ndiyo siku pekee ambayo utaona kifo ndio kitu pekee kinacho kifaa, sababu nimeona uwezikuacha kuni fwatilia” ilisikika sauti upande wapili wa simu.

Nyondo anazidi kujawa na hasira, lakini kabla ajasema lolote, ikasika tena sauti toka upande wapili wa simu, “lakini kama uto jari, nakusubiri kwenye ofisi za Tino Nyondo Trans, nakushauri hakikisha unakujana vijana wakutosha, maana ulio nao awawezi kukulinda ata kidogo, au chagua kubakia nyumbani, ukisubiri kinachofwata….” ata kabla upande wapili aujamaliza kuongea, tayari Tino Nyondo alisha kata simu.

“Kichondo, kawaambie vijana tuonaondoka sasa hivi” alisema Nyondo huku anatembea kuelekea nje upande wa mbele, kule kwenye waombolezaji, “sawa boss” aliitikia Kichondo, huku anaondoka na kuelekea upande wa nyuma wa nyumba.

Nyondo anaibukia upande wa mbele, nakuanza kutembea kuelekea kwenye maegesho ya magari, mtu mmoja anamfwata Nyondo kwa haraka, “vipi mzee, kuna taarifa yoyote ya kuwajulisha waombolezaji?” nauliza yule mtu, “mazishi kesho saa saba, naenda kumchukuwa huyo mshenzi” alisema Nyondo, ambae nikama alikuwa na uhakika wa kuwa, wa kile anacho kisema.

Yule jamaa anatoa macho kwa mshangao, na kusindikiza Nyondo kwa macho, ata alipoingia kwenye gari, na dereva anaondoa gari kuelekea nje geti, sasa kila mmoja pale ndani akilitazama lile gari.

Sekunde chache mbele yanasikika magari mengi sana, yakiunguruma, tokea upande wa nyuma wa nyumba, kisha yakaanza kutembea kuelekea nje yauzio na kushika uelekeo wa mjini, yakiungana na gari la Nyondo.

“kumekucha, leo lazima tusikia kitu” alisikika mtu mmoja akiongea kitu ambacho kila mmoja alikuwa anakiwaza, maana mwonekano wa msafara ule wa bwana Nyondo, aukuwa wa kawaida.****

Mida ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, walikuwa wanasimamisha gari dogo aina ya Hyundai, mbele ya kituo kikuu cha polisi, kisha wakashuka, “tupumzike bwana askari wengi wapo doria, watatupa taarifa za kinachoendelea huko mtaani” alisema ASP Ayoub Mzee, wakati wanashuka toka kwenye gari.

“muda umeenda sana, hapawezi kutokea kitu chochote, nazani yule kaka, ameamua kukimbia nje ya mji” alisema Insp Aisha, ka sauti ya kupooza, vipi lakini, mbona kama umekosa amani?” anauliza ASP Ayoub Mzee, huku wanatembea kuingia ndani ya jengo la makao makuu.

“sijuwi kwanini, lakini namfaikilia sana yule kijana, naona kama alifanya jambo sahihi kumuuwa Lukas, siume ona walichotaka kunifanyia, wale ni watu hatari sana” alisema Insp Aisha.

“lakini kupatikana kwake, ndio usalama wa familia yangu” alisema Ayoub Mzee, akionyesha kuwa, anatamani muuwaji wa Lukas apatikane, ili na yeye ajiweke salama, mbele ya Nyondo.

“usizani kuwa ni kazi lahisi kumkamata yule kijana, na hakika kunavifo vitaongezeka, na usishangae ukasikia kuwa polisi wetu wamepatwa na bahati mbaya” alisisitiza Insp Aisha, kwa sauti iliyo jaa maonyo, na tahadhari.

Wakati huo walikuwa wameshaanza kupanda ngazi, za kuingia mapokezi, “unamaanisha kuwa, anaweza kuwa hatari zaidi ya Nyondo?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, huku anasimama na kumtazama Insp Aisha, ambae nae anasimama pia.

“sikutanii afande Ayoub, yule kijana ni hatari sana, alichinja watu watatu kwa sekunde mbili” alisema Insp Aisha, na kumfanya ASP Ayoub Mzee aache mdomo wazi kwa mduwao, “weeeee!, unasema ukweli?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, akionyesha mshangao wawazi kabisa.

“sasa je, unazani ilikuwaje kule chuoni, aliwakata shingo zao, kama mbuzi wagonjwa, na akutumia risasi ata moja” alisema Insp Aisha, akimsimulia ASP Ayoub Mzee kile kilicho tokea, wakati yeye amepoteza fahamu.

“dah!, kama ni hivyo basi kazi hipo, ndio maana mpaka sasa awajampata, ujuwe ni ajabu, kwa Nyondo kuangaika hivi kumpata mtu alie mkusudia” alisema ASP Mzee, huku wanaendelea kupanda ngazi, na kisha kuingia ndani ya jengo, ambako waliibukia mapokezi, ambako waliwakuta askari wawili.

“afande afadhari umefika, maana sasa hivi, imengia taarifa kuwa, Nyondo na vijana vijana wake wamtoka mateka, wanaelekea mjini, inaonyesha kuna tukio wanaenda kulifanya” alisema mmoja kati ya wale askari wawili waliokuwepo mapokezi.

Ukweli hapo ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, awakusubiri kuambiwa mala mbili, haraka sana wakatoka nje na kuingia kwenye gari lao, walilokabidhiwa na jeshi la polisi, kwa kazi mahalumu, na kuondoka zao kuelekea mjini.

Lakini basi, ile wanaingia barabara kuu, itokayo mikoa ya kusini, wanashtuka wanaona msafara wa magari zaidi ya ishilini, yakipita mbele yao kwa mwendo mkali, yakielekea mjini, “kumekucha, huyu jamaa kapania kweli kweli” alisema ASP Ayoub Mzee, ambae alipanga mala baada ya magari aya kupita, basi na yeye atawafwata kwa nyuma.***

Mida hii mwana dada Anastansia, alikuwa ametulia kwenye shimo la Panya, akimsubiri mpenzi wake Hance, ambae alimwambia kuwa, kuna jambo alikuwa anaendea kuliweka sawa, kisha waje kupumzika.

Lakini ukweli ni kwamba, mida hii maeneo ya Songea mjini, jilani na stend kuu ya mabus yaendayo mikoa mingine pamoja na jijini dar es salaam na nchi za jilani, kama vile msumbiji na #Mbogo_Land, tuna zungumzia eneo lililopakana na kanisa kuu la mkoa.

Ili ni eneo la KAURU ya zamani, ambapo sasa palikuwa pana milikuwa, kampuni ya Tino Nyondo Trans, ni eneo ambalo upande wambele ungeona jengo kubwa la ghorofa moja, ambalo mida hii, lilikuwa kimya kabisa, tofauti na kawaida yake, ka wale wanao lifahamu. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata