
SEHEMU YA THEMANINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NNE: Ili ni eneo la KAURU ya zamani, ambapo sasa palikuwa pana milikuwa, kampuni ya Tino Nyondo Trans, ni eneo ambalo upande wambele ungeona jengo kubwa la ghorofa moja, ambalo mida hii, lilikuwa kimya kabisa, tofauti na kawaida yake, ka wale wanao lifahamu. ….ENDELEA…..
Maana mida hii, ungewaona au kusikia sauti za walinzi, wakiongea ili na lile, na wengine wakitembea na kuzunguka huku na huku, kuhakikisha usalama wa eneo lile, ambalo lina mali nyingi na vitu vya thamani vya bwana Tino Nyondo.
Ukiachilia computer na nyaraka nyingi za kifedha zilizopo ndani ya jengo ilo, pia kulikuwa na chumba kikubwa kinachotumika kama benk ndogo, ya kuifadhia fedha za kampuni hii, inayoongoza kwa utowaji wa huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa mikoa ya kusini, na nyanda za juu kusini.
Pia upande wa nyuma wa jengo, kulikuwa na eneo kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa sana, ndani yake kukiwa na magari zaidi ya themanini, kati yake magari sitini yakiwa ni makubwa ya mizigo.
Lakini basi, Mita mia tatu, toka lilipo jengo la kampuni ya Tino Nyondo trans, upande wa kusini, yani kwenye barabara inayo tenganisha kanisa na kituo cha redio cha kanisa ilo la kikatoriki, pana onekana BMW rangi nyeusi, likiwa limesimama, chini ya mti mmoja uliojifunga vyema, kwa matawi yake.
Ndani ya gari anaonekana mwanadada Farida, ambae alikuwa ameweka darubini machoni mwake, akishikilia kwa mkono wa kushoto, na kuielekeza kwenye jengo la kampuni ya Tino Nyondo Trans, mkono wake wa kulia, ameshikilia redio ndogo ya mawasiliano.
“bado meza ni nyeupe, wapita njia nao wamepungua” anasema Farida, ambae pembeni yake kulikuwa na silaha aina ya MM12 sniper, “ok!, kipepeo, utajulisha mala moja, ukiona kitu, kumbuka kiwashio kipo dirisha la tatu, toka kushoto kwako” ilisikika sauti ya kiume toka kwenye redio.
“nimecopy Panya, cha msingi, kaa mbali na chumba cha tatu” alisema Farida, akiwa amesogeza ile redio aina ya Motorola, karibu na mdomo wake, darubini anaishusha toka kwenye macho yake.
Lakini basi, wakati huo huo, anasikia miungurumo ya magari zaidi ya moja, yakija upande ule, kutokea katikati ya mji, sambamba na mwanga wa taa za magari hayo.
Haraka Farida anarudisha darubini macho, huku anasogeza redio mdomoni, “Panya unanisikia?” anauliza Farida, huku anatazama upande wa jengo la Tino Nyondo Trans, “nakupata kipepeo, vipi kuna ujumbe mzuri kwangu, maana naanzakusikia kelele za farasi tokea upande wa sokoni” ilisikika sauti ya kiume redioni.
Hapo Farida anashuhudia magari mengi mchanganyiko, yakiingia pale Tino Trans, na kuingia moja kwa moja upande wa nyuma wa eneo ili, na magari machache yakiingia upande wambele, ambako geti lilikuwa wazi.
“kaka Panya, kama unavyo sikia ndivyo ninavyo ona, kazi tuliyo itamani, hii hapa imesha wadia, magari zaidi ya ishilini yanakuja hapo mjengoni” anasema Farida ambae kwa msaada wa kiona mbali anamwona bwana Tino Nyondo Nyondo na mlinzai wake Kichondo, wanashuka toka kwenye gari, sambamba na vijana kumi na mbili, walioshuka toka kwenye magari matatu, waliyokuja nayo.
“nimeyaona magari yana ingia upande wa uwani, wacha kwanza nianze kumlegeza Nyondo, kisha nimmalize kilaini kabisa” ilisikika sauti ya kiume, toka upande wa pili wa simu, “kila lakheri Panya” alisema Farida kisha akachomeka simu kwenye mkanda wa suruali aliyokuwa ameivaa, na kuinua bunduki yake, ya kudungulia, alafu akaielekezea kwenye jengo la Tino Nyondo trans, akitumia kioo cha mlango alichokuwa amekishusha.***
Naaaaaaaaam!, mita sitini toka kwenye jengo la Tino Nyondo trans, upande wa mashariki, yani upande wa mjini, ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha Amary, waliovalia mashati mepesi ya vishikizo, na suruali nadifu za vitambaa, zilizo wapendeza na kuwakaa vizuri, walikuwa ndani ya gari lao, aina ya Hyundai, walilolisimamisha pembezoni mwa safu ya maduka, ambayo sasa yalikuwa kimya kabisa.
Wawili awa walikuwa wametulia ndani ya gari, macho yao wameyaelekeza kwenye ofisi za Nyondo trans, “sijuwi wanataka kufanya nini awa jamaa, alafu mbona polisi wengine siwaoni” anauliza Insp Aisha, huku anatazama kushoto na kulia.
“nazani bado awajapata taarifa, maana sisi ndio wakwanza kupewa taarifa” alisema ASP Ayoub Mzee, ambae alikuwa anatazama kule kwenye ofisi za bwana Tino Nyondo.
Wakati huo wanasikia sauti ya Tino Nyondo akitoa maelekezo kwa watu wake, “hakikisheni atoki humu ndani huyu mshenzi” ilikuwa ni sauti ya juu yenye hasira.
“kumbe yule kijana yupo mle ndani, afande, inabidi tufanye jambo la haraka sana, wanaweza kumuuwa” alisema Insp Aisha, “lakini wakimuuwa ndio unafuu wetu, vinginevyo tutaendelea kuwa katika hatari” alisema ASP Ayoub Mzee.
“lakini afande kumbuka yule kijana aliniokoa, ata ilo alitoshi kukufanya angalau uone anaitaji kuishi?” anauliza Insp Aisha, ambae anatazama upande wa kushoto, na kuona kibanda cha kupigia simu, maarufu kama call box.
“ni sawa Aisha, lakini atuna uwezo wa kumsaidia, na wakati mwingine, maisha ni kombolela, inafaa kutoa sadaka moja, ili wengine wapone” anasema ASP Ayoub Mzee, na wakati huo huo anasikia mlango wagari unafunguliwa, anapotazama upande wake wa kushoto, anamwona Insp Aisha anashuka toka kwenye gari.
“unaenda wapi sasa?” auliza ASP Ayoub Mzee, huku anamtazama Insp Aisha, “naenda kupiga simu kituoni, nitoe uelekeo sahihi, ili tuongezewe msaada” alisema Insp Aisha, huku anatembea kulifwata call box, wakati huo anajipapasa mfukoni, kuangalia kama ana card ya kupigia simu.
“Aisha amekuwa wa ajabu sana, mbona kama anamchukulia huyu muuwaji kama mtu mwema” anasema ASP Ayoub Mzee, huku anageuza uso wake kutazama kwenye jengo la Tino Nyondo trans, ambako sasa anamwona Tino Nyondo anaonekana akiwa amesimama karibu na mlango anatazama eneo lile, huku amekasirika kweli kweli.
Wakati huo sasa, upande wa nyuma wa jengo la ofisi za Nyondo, vijana wanashuka toka kwenye magari na slaha zao mikononi, wanatawanyika kwa haraka na kuzunguka eneo lote la maegesho ya magari, na wengine wanaelekea upande wa jengo kubwa la ofisi.
Kule kwenye jengo la ofisi sasa, bwana Nyondo anashtushwa na ukimya uliopo, hakuna mlinzi yoyote anae onekana, wakati kikawaida, uwa akiingia tu, lazima walinzi wa eneo lile wangu sogelea na kumsalimia.
Lakini leo mpaka bwana Tino Nyondo anafika mlangoni, hapa kuwana dalili ya mtu yoyote kuwepo eneo lile, zaidi ya wao waliokuja, “Kichondo, kagua eneo, lote, maana sioni dalili ya kuwepo walinzi” alisema Tino Nyondo, ambae mkononi mwake, alikuwa ameshika fimbo yake mkononi.
Kichondo anageuka nyuma, ambako wapo vijana kadhaa wwenye bunduki tofati tofauti, kama vile SMG, MODOEL 81 na zile za kipimo cha kati, yani PKM, na minyororo ya risasi zake zenye mzingo wa mm7.62, kwa wasiyo ifahamu au kama umeisahau, inaitwa Pure Korkonshiv Machine Gun, wengi uiita medium machine gun au MMG, iliyo undwa kwa mala ya kwanza, mwaka 1947, na askari wa Rusia, major Korkonshov, ambae pia ndie mbunifu wa silaha aina ya AK-47, ikifwatiwa na mataifa meingine kutengeneza silaha mbali mbali kwa mfano wake, ikiwa pamoja na SMG ya mwaka 1956 na 1957.
“nyie nifwateni, na nyie watatu bakini na boss” alisema Kichondo, akiwagawa vijana katika makundi mawili, wawengine wakisogea kwa bwana Tino Nyondo, hku wengine wakimfwata Kichondo, ambae alianza kutembea, kuelekea kwenye vibanda vya kupumzikia walinzi. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU