
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO: “nyie nifwateni, na nyie watatu bakini na boss” alisema Kichondo, akiwagawa vijana katika makundi mawili, wawengine wakisogea kwa bwana Tino Nyondo, hku wengine wakimfwata Kichondo, ambae alianza kutembea, kuelekea kwenye vibanda vya kupumzikia walinzi. ….ENDELEA…..
Wakati huo huo, Nyondo na vijana kama watatu hivi, wanatembea kuingia ndani ya jengo, “huyu mpuuzi, atakuwa amekaa wapi?” anasema Tino Nyondo, huku anatembea kwenye kolido na kuzifwata ngazi za kuelekea ghorofa ya pili, sambamba na vijana wake.
Huku nje nako Kichondo, analifikia banda la kwanza la walinzi, ambapo ile anaingia tu, anakutana na kichwa cha binadamu, kikiwa mlangoni, anapopeleka macho mbele kidogo, anaona kiwili wili, chenye mavazi ambayo, ni sare ya nguo nyeusi, kwamaana suruali na tishert, kikiwa kimelala chini, katika dimbwi la damu.
Kichondo anatoa macho kwa mshtuko, huku anatazama pembeni, macho yake yakifwatilia jito kidogo cha damu, ambako pia anakutana na watu wawili, walio lala chini, huku shingo zao zikiwa na jelaha kubwa, zenye kuchuluzika damu.
“huyu mpuuzi anawezaje kufanya hivi?” aliuliza Kichondo kwa sauti ya mshtuko, huku anatazama nje ya kibanda, ambako anawaona baadhi ya vijana wao, wakija upande wa mbele, wakitokea upande wa nyuma, yani kwenye maegesho, na bunduki zao mkononi.
“nyie mnakuja kufanya nini huku, ebu tawanyikeni, na muhakikishe huyu mpuuzi anakamatwa haraka” alisema Kichondo, kwa sauti ya kupayuka, huku anatoka kwenye banda la walinzi.
“jamani heee!, njooni muone, kuna walinzi wameuwawa huku” anasikika mmoja kati ya vijana wa nyonto, akipiga kelele toka upande pembeni ya ukuta wa kushoto wa jengo ilikubwa.
Wote wanakimbilia upande huo, lakini kabla awajafika sehemu hiyo, mala wanasikia tena ukelele, “jamani huyu hapaaaa….,” ilikuwa nisauti kali ya juu, iliyo shindwa kumaliza kufikisha ujumbe, kwamaana ilikoma ghafla, na kuwashtua zaidi wenzake, ambao waliongeza mwendo, kukimbilia upande ule, huku bunduki zao zikiwa tayari kwa mashambulizi.
Naaaam!, baada ya hatua chache waliotangulia wanaibukia eneo lile, huku wanamwona mwenzao, akiwa amelala chini, anatapatapa, shingoni kwake kukiwa na jelaha kubwa, na damu nyingi zikimtoka kwenye jelaha ilo.
Ile wanatazama mbele, upande wa maegesho yenye magari mengi ya mizigo, wote kwa pamoja wanamwona mtu alie valia jacket jeusi, anapotelea gizani, “oyah!, mkimbizeni huyo mtu, hakikisheni atoki hapa” alisema Kichondo, kwa sauti ya juu yenye kuamrisha.
Na hapo vijana wanachomoka mbio, kukimbilia kwenye maegesho, ambako kulikuwa na gizani nene, “wengine wapite upande wakulia” alisema Kichondo, uku wanaendelea kukimbia, kuelekea upande wa maegesho.
Wakati huo huo, jamaa wengine walio kuwepo kule maegesho ya magari makubwa, tayari walikuwa wamesha sikia zile kelele za wakina Kichondo, nao walishaanza kukimbilia upande wa mbele, waliokuwa wanakimbilia wenzao,.
Ata walipokutana kati, na kujikusanya watu zaidi ya therasini, awakumwona mtu waliemkusudia, “ameingilia wapi huyu mshenzi” anauliza Kichondo, kwa sauti yenye jazba, “mkuu, nivyema kama tukitawanyika kumtafuta” alisema mmoja wao.
“aya!, wote tafuta humu ndani, hakikisha unacharaza risasi, kila unacho kiona, kuanzia mijusi, mpaka binadamu ambae ni tofauti na sis…” Kichondo akuweza kumaliza kauri yake,.
Maana ghafla walisikia mchakato wa nyayo nyepesi, kama zap aka au chui, ile wanageuka kutazama upande wao wa kulia, wanamwona mwenzao mmja akianguka kama kifurushi kilichokosa kiegemeo, kichwa kinaenda kwake, na mwili unaenda kwake, vijana wanaingiwa na bumbuwazi, lenyeuoga mwingi ndani yake.
Wakati huo huo wanamwona mtu alie valia suruali nyeusi na jacket jausi, akikimbia kuingia kwenye upenyo wa kati ya gari na gari, “shambuliaaaaaaa!” alipiga kelele Kichondo, bila kufikiri mala mbili.
Hapo sasa, kitendo bila kuchelewa, vijana wanainua bunduki zao, na kuelekeza kule ambako, walimwona mtu yule anakimbilia, kila mmoja aliamini kuwa, akizubaa kushambulia, basi yeye ndiyo atapitiwa na mdudu huyu mwaribufu.
Wakati huo huo, ndani ya jengo ili kubwa, ghorofa ya pili, tuna waona vijana, watatu wenye silaha, wakiwa wamesimama kwenye kolido, usawa wa chumba kimoja chenye lango la chuma, lililokuwa limefungwa.
Sekunde chache baadae mlango unafunguliwa, anaibuka bwana Tino Nyondo, na na kutupa nafasi ya kuchungulia ndani, ambako kwa macho yetu tunaweza kuona makabati ya vioo, yaliyo pangwa pembezoni na kati kati ya chumba iki kikubwa, kuanzia chini mpaka juu.
Ndani ya makabati hayo, ndani yake kuilionekana mabunda ya fedha, noti za elfu kumi kumi, zikiwa za rangi ya blue, kamaungeona, usingefikiliakuwa ni fedha za kweli, kutokana naauwingi wa fedha zile.
Sasa basi, wakati Nyondo anafunga mlango, mala wakaanza kusikia milipuko mingi ya risasi toka nje ya jengo lile, upande wa maegesho ya magari, “tatari mwamemwona huyu mshenzi” alisema Nyondo, huku ana piga hatua za haraka, kuelekea kwenye mlango wa chumba cha upande wa pili.
Nyondo anajaribu mlango wa kwanza, anakuta umefungwa, anajaribu wa pili hivyo hivyo, mpaka anapo kuta mlango wa tatu, wa chumba ambacho wafanya kazi ubadirishia nguo, anaukuta ukiwa wazi.
Yeye na vijana wake wanaingia ndani, na moja kwa moja wanakimbilia dirisha, na kutazama nje kwa chini, ambako milindimo ya risasi ilikuwa inaendelea, bunduk i mbali mbali zikikooa, huku PKM wengi wanaita mjegeja, ikisikika zaidi, na kupendesha tukio.
“kum… make…” Nyondo anaachia tusi la nguoni, hakika alicho kiona ni kitu ambacho akukitarajia kabisa, ni zaidi ya asivyo tarajia, “nyie washenzi mnaaribu magari yanguuuuuu” alipiga kelele Nyondo, ambae aliona jinsi risasi, zilivyo kuwa zina gonga kwenye magari yake makubwa ya mizigo, na kuboa sehemu mbali, ikiwepo kupasua vioo, na mwili wa gari, huku wakati mwingine, wakitoboa magurudumu ya magari hayo.
“nyie wapumbavu acheni kupiga ovyo risas…..” Nyondo akupata nafasi ya kumaliza kile alichokuwa anakiongea, maana ulitokea mlipuko mkubwa ulioenda sambamba na vipande vya mwili wa gari kutupwa hewani, na na baadhi ya vipande vya moto vina shukia kwenye magari mengine, ambayo pia yanaanza kushika moto. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU