
TOBO LA PANYA (88)

SEHEMU YA THEMANINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA: Wakati huo Hance akiwa hewani mikono ikizama kwenye koti lake, na kuibuka na visu viwili vya kukunja, ile anatuwa chini katikati ya kundi la wale jamaa wanne, tayari wawili kati yao walikuwa wamesha shikilia shingo zao, na kuanguka chini kama viroba, huku damu zina mwagika toka kwenye majelaha makubwa shingoni mwao. ….ENDELEA…..
Kuona hivyo wale wengine wakaona wakizubaha, watachinjwa kama mbuzi wa kafara, hivyo mmoja anainua bunduki yake kama gongo la mti, na kuishisha kwanguvu, akilenga kichwa cha Hance.
Lakini akiwa amekosa bahati, akamwona kijana huyu, akibonyea kidogo na kupishana na ile bunduki, ambayo ilipiga kichwani mwake sentimita chache sana, lakini akahisi kitu chenye ncha kali kama wembe, kikipita tumboni mwake.
Yule jamaa mwingine, anatazama tumbo la mwenzake, anaona tumbo la mwenzie likiwa limeachama na utumbo una mwagika nje, kama mfuko ulio chanika ghafla.
Jamaa akaona hii ni zaidi ya hatari, lakini kabla ajafanya lolote, tayari Hance alikuwa karibu yake anakuja mbio mbio, na kabla ajaamua la kufanya, tayari kijana Hance alikuwa anapita mbele yake, huku kisu cha kukunja kikpita shingoni kwake kwa uharaka na wepesi wa ajabu, sidhani kama naweza kuelezea alicho jihisi, maana tayari kichwa na kiwili wili vilisha tengana.
Lakini basi, Hance nae akiwa katika mwendo, anakatika kwenye penyo za magari, mala ghafla anakutana na kundi la watu kumi mbele yake, nao wakiwa na bunduki mikononi mwao.
Ile anageuka ili akimbilie upande wapili, nako akawaona watu wengime wamakuja mbio mbio, lakini wote wakiwa wameinamisha bunduki zao, ni wazi walisha ishiwa risasi, na ungeliona ilo, kwakutazama ile MMG, maana aikuwa na mkanda wa risasi ata moja.
Hance alie shikilia visu vyake vya kukunja, ambavyo vilikuwa vina vuja damu nyingi, akatulia na kuwa tazama awa jamaa, ambae tofauti na utaratibu wao, maana mpaka dakika hii, lazima wangekuwa wamesha mshambulia kwa risasi nyingi.
Jamaa wanamtazama Hance kwa tahadhari, kama vile wanamkagua, kijana huyu, ambae mpaka sasa amesha sababisha robo tatu ya wenzao, kupoteza maisha, kwa risasi na kuwachinja.***
Huko nje ya upande wa mashariki, mita sitini toka kwenye jengo la Nyondo trans, Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee, wakiwa ndani ya gari, baada ya kusikia milipuko mingi ya risasi, na magari yakiwaka moto.
Sasa wanaona milipuko ya risasi imekoma, japo moto ulikuwa unaendelea kuwaka, kelele za watu waliokuwa wanapiga kelele za machungu ya vifo, sasa zimekoma,.
“awa watu mbona wanachelewa kuja, afande amesema watapewa taarifa haraka” alisema Insp Aisha kwa sauti yenye kulalamika, akionyesha kuwa na wasi wasi wawazi kabisa, “Aisha unanini lakini, ujuwe ata wakuu wenyewe wanataka huyu dogo afe, ili hasira za Nyondo zitulie” alisema ASP Ayoub Mzee, na kumfanya Insp Aisha amtazame, kwamacho ya mshangao.
“hivi unajisikia unacho oongea, unamaanisha akifa yule kaka, ndio utakuwa mwisho wa manyanyaso na ubakaji wa bwana nyondo, au unazani familia yako itakuwa salama siku zote?” aliuliza Insp Aisha, huku akimtazama ASP Ayoub Mzee.
ASP Ayoub Mzee anatulia kwa sekunde kadhaa, nikama alikosa jibu la kumpatia Insp Aisha, “tusiwe kama wao, wamelea maovu, sasa wanatafuta pakutokea” anasema Insp Aisha, na ASP Ayoub Mzee anakuwa kimya, anampa nafasi Insp Aisha ya kuendelea kuongea.
“ebu ona unazani kesho, taarifa zinaendaje makao makuu dar es salaam” anauliza Insp Aisha, na bado Ayoub Mzee, anaendelea kukaa kimya, ni wazi hataki kabisa kukubariana na Insp Aisha.
Kule ndani ya jengo lenye ofisi, mzee Nyondo, anaonekana kuzidi kujawa na hasira kali sana, kwanza magari yake yote yameshambuliwa na vijana wake mwenyewe, pili kundi kubwa la vijana wake, wamesha uwawa, japo hii aikuwa tatizo kwake, maana kwa fedha alizokuwa nazo, angenunua magari mengine na kutafuta vijana wengine.
“hivi wanashindwaje kumdhibiti mtu mmoja awa wajinga” anauliza mzee Nyondo ambae anatembea kushuka chini, akiongozana na vijana wake watatu, “boss, sizani kama huko chini nisalama kwako” alisema mmoja kati ya wale vijana watatu.
“sijari kuhusu hatari, ninavijana wengi, inakuwaje niofie kuhusu mtu mmoja” anasema mzee Nyondo kwa sauti yenye hasira, huku anamaliza ngazi na kuanza kutembea kupita aneo la wazi, la mapokezi,a ambalo sasa alikuwa na mtu yoyote, wakifwata mlango wa kutokea nje.
Vijana wanatazamana, kama wanaulizana tufanyaje, kisha wanaonyesha ishala ya kuwa watulivu, na kuendelea kumfwata boss wao, ambae anatoka nje na kuelekea kwenye gari, “sasa ni wakati wakazi, siwezi kuacha huyu mjinga anichezee” alisema mzee Tino Nyondo.
Wakati huo huo, Farida alikuwa ndani ya gari, anamtazama bwana Nyondo, kwakutumia kilengo cha bundi yake aina ya MM12 sniper, ambapo anamwona Tino Nyondo, akiwa analifikia gari lake na kufungua mlango, kisha anatoa AK-47.
Wakati huo milipuko ya risasi, ilikuwa imekoma, lakini mwanga mkali wamoto, unaonekana toka upande wa nyuma, wa ofisi za bwana Nyondo, “Farida anaminya kitufe cha PTT, kwenye redio yake, kisha ana isogeza mdomoni, “kaka Panya, naona mzee Nyondo anaingia kazini mwenyewe, naona anachukuwa model 81” anasema Farida, huku macho yake yakiwa kwenye kilengeo cha bunduki.
“wamenibana vibaya sana, sijuwi wamekuja wangapi, naona awaishi” anasikika Hance akiongea toka upande wapili wa redio, sasa milipuko ilikuwa imesha tulia.
“kwahiyo hali ni mbaya sana kaka Panya, niambie nifanye nini?” anauliza Farida kwa sauti yenye shahuku, “tulia kwanza nipo katika kipindi ambacho nakipenda sana” aliskika Hance toka upande wapili wa redio. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

