TOBO LA PANYA (90)

SEHEMU YA TISINI

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TISA: Bwana Nyondo alimiani maneno ya kwenye ule ujumbe, kwamba akae mbali na kijana huyo, kwamba ni mtu hatari sana, “shambulieni” alipiga kelele Nyondo, huku anageuka na kukimbilia kule alikotoka, yani upande wa mbele wa jengo la ofisi zake. ….ENDELEA…..

Vijana wake wanapiga risasi ovyo bila kumwona adui yao, mpaka walipo kuja kutahamaki, kijana yupo nyuma yao, na ile wanageuka, tayari kijana alikuwa anapita na shingo zao.

Na wakati huo huo, redio yake ikasikika, mita chache toka kwenye jacket, “kaka Panya, naomwona Nyondo anakimbilia kwenye gari lake, nipe kibari cha kumzuwia” ilikuwa ni sauti ya Farida.

Hance anawai jacket lake na kuichukuwa redio ambayo bado ilikuwa kwenye ukosi wake, nakuisogeza mdomoni, akiminya PTT, “fanya hivyo kipepeo, anza na dereva kisha washa chumba cha tatu, ghorofa la pili” alisema Hance kisha akaanza kutembea kwa tahadhari kuelekea upande wambele wa jengo lile kubwa.

Naaaaaaam!, Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee, bado wapo kwenye gari, wametoka kusikia milipuko mingine ya risasi, sasa wanamwona Nyondo anakimbilia kwenye gari, “inamaana wakuu wamewazuwia askari wasije huku?” anauliza Aisha, kwa sauti yenye kuchukia.

“nilisha kuambia Aisha huyu kijana ni tatizo kubwa, unazani Nyondo baada ya hapo atafanya nini, lazima ajipange na kuanza kutushambulia sisi na raia wema, wasio na hatia” alisema ASP Ayoub Mzee mzee ambae anaamini kuwa kifo cha Hance ni salama ya familia yake.

“kama unaamini hivyo kaka Mzee, basi unakosea sana” anasema Insp Aisha, huku wanamtazama Nyondo ambae analifikia gari lake kwa haraka, “washa gari haraka tuondoke” anasema Nyondo, huku anafungua mlango wa gari na kuingia ndani kwa haraka.

Lakini anashangaa kumwona dareva ametulia pasipo akujiangaisha kuwasha gari, Nyondo anapiga kiegemeo cha seat ya dereva, “we mpuuzi nasema washa gar…..” alisema Nyondo kwa sauti yenye hasira na ghadhab, lakini ghafla anakugunduwa kuwa, kiegemeo cha seat ya dereva, kilikuwa kimelowa, anapo inua macho yake anaona tundu kubwa kwenye kioo cha mbele kilicho tengeneza nyufa kama tandabuhi.

“mamaaaaaa!” anapiga kelele Nyondo, huku anafungua mlango na kutoka nje yagari, bundiki ameiacha ndani ya gari, anaanza kukimbilia ndani ya nyumba, “mzee unakimbia nini, mbona wewe ni jasiri na mkatili sana” ilisikika sauti toka upande wa kulia wa jengo.

Nyondo anageuka na kutazama upande ulio tokea sauti, anamwona kijana mmoja wa kawaida tu, alie valia tishert nyeupe yenye kulowa damu, visu viwili mkononi, visu vya kukunja, visu ambavyo ameiona kazi yake, na wakati huo huo vinasikika ving’ora vya magari ya polisi, yakija upande wao.

Nyondo anasimama, na kugeuka upande huo, “we mshenzi unataka nini?” anauliza Nyondo, ambae sasa alionekana wazi kuwa katika hali ya uoga, uliopitiliza, “nataka nimalize ili swala” alisema Hance kwa sauti tulivu kiasi.

“unamalizaje, umemuuwa mdogo wangu, umearibu magari yangu” alisema Nyondo ambae ukiachilia uoga wa mwanzo, sasa alionyesha kuwa na hasira, “nimesikia unaitaji mtu, wakumsindikiza mdogo wako kaburini, unaonaje ukiwa wewe” anasema Hance kama vile anatania.

“Nyondo anatazama upande washariki, anaona mianga ya magari ya polisi, ambayo yalikuwa yanazidi kusogea, “najuwa hauna fedha ya kuwa polisi, wakati mimi jinalangu tu, linatosha kuniweka huru, isitoshe ninafedha” alisema Nyondo kwa sauti ya dharau.

“mh!, unazani ni lahisi kuogopwa na jeshi la polisi, wakati sasa hauna watu?” aliuliza Hance kwa sauti ile ile tulivu, na kumfanya Nyondo acheke kidogo, “ninafedha kijana, ninauwezo wa kupata chochote, na kumpata mtu yoyote ninae mwitaji” alisema Nyondo, kwa sauti ya kujiamini.

Safari hii ilikuwa zamu ya Hance kuachia kicheko kifupi, “fedha unazungumzia fedha zipi mzee Nyondo, au zile” anasema Hance huku anatazama upande wa kushoto wa jengo kubwa, uasawa wa ghorofa ya pili.

Inamshtua sana Nyondo, anashindwa kuelewa kijana huyu amejuwa juu ya ifadhi yake ndogo, anageuka na kutazama upande ule, ambako anakuitana na kitu cha kushtusha, kama siyo kufurahisha.

Muda huo huo unasikika mlio kama wa kuvunjika kwa kioo, kisha inafwatiwa na mlipuko mkubwa, kwenye chumba cha tatu, ghorofa ya pili, sambamba na kuopnekana kwa vipande vya karatasi vikipepea hangani, huku vinawaka moto.

“mamaaaaa fedha zanguuuu” anapiga kelele bwa Nyondo, huku anatazama tukio lile la kuumiza moyo wake, kabla ajageuka na kumsogelea kwa haraka Hance, ambae anamsubiri amfikie tu, nae anazamisha kisu tumboni mwa mzee Nyondo.

“nivyema ukasahau kuhusu fedha, zaidi ya kusubiri kuzikwa pamoja na mdogo wako, kama ulivyo taka” alisema Hance kwa sauti tulivu ya taratibu, huku bado ameshikilia kisu kilicho zama tumboni kwa Nyondo.

“hapa….. hapa…… hapana, usini ……. uwe” alisema Nyondo huku anaanza kutokwa damu mdomoni, “ulichelewa kusema hivyo, ilifaa uniambie mapema sana” alisema Hance huku anapeleka mkono wake upande wa kushoto wa tumbo la Nyondo, na kisu kinatokea upande huo kikiwa kimechana kabisa tumbo la mzee huyu, na utumbo unatawanyika kabisa, na kudondoka chini, sambamba na damu nyingi sana.

Kisha Nyondo nae anafwata kwenda chini, kama zigo la pumba za mtazama, na kuanza kunyosha nyosha viungo vyake, kama kuku anae kufa kwa pigo la jiwe la kichwa.

Baada ya hapo Hance anachukuwa redio yake, na kubofya push to talk, yani PTT, “kipepeo, cha kwa haraka, ingia ndani chukuwa kila kilicho cha kwangu, tutakutana shimoni, nikiwa nimesha malizana na polisi” alisema Hance kisha akaweka visu chini, pamoja na ile redio, ambayo ilikuwa inamaliza kusikika, “nimecopy Panya, najuwa hakuna gumu mbele yako” alisikika Farida, huku Panya akipotelea kwenye lango la uzio wa ofisi za Nyondo.

Naaaaaaaam!, Hance anatoka nje ya geti, ambako anayaona magari mengi ya polisi, “hupo chini ya ulinzi, weka silaha yako chini, na unyooshe mikono juu” ilisikika sauti ya askari wakike, yenye kusikika vyema.

Hance au SA-26, ananyoosha mikono juu, kwamaana hakuwa na silaha yoyote mkononi, “hakuna piga risasi, na rudia tena, hakuna kupiga risasi, mtuhumiwa ametihii amri” Hance anaitambua sauti hii ya kike, ni ya mwanamke alie mwokoa kwa Nyondo. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!