TOBO LA PANYA (91)

SEHEMU YA TISINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI: Hance au SA-26, ananyoosha mikono juu, kwamaana hakuwa na silaha yoyote mkononi, “hakuna piga risasi, na rudia tena, hakuna kupiga risasi, mtuhumiwa ametihii amri” Hance anaitambua sauti hii ya kike, ni ya mwanamke alie mwokoa kwa Nyondo. ….ENDELEA…..

Askari wanakimbia kumsogelea, wanapo mfikia wanamfunga kwa bangiri za chuma, yani pingu, huku mitutu ya bunduki zao ikimtazama kijana huyu, ambae kila polisi alie mwona alimtazama kwa mshangao, huku moyoni akijiuliza, “mtu mwenywe ndiyo huyu”.

Polisi awakujari, kuhusu mwanamke aliekuwa anatembea kueleka upande wapili wa barabara, yani uapnde ambao jengo la bwana Nyondo lipo, nazani sababu alipita kwa nje.

Askari wanamsindikiza Hance kwenye gari, huku zinapita dakiak kama tano saba hivi, za kumkagua na kumpakiza Hance kwenye gari, ndipo ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha wakikumbuka kitu, “askari wengine wakakague mle ndani” anasema Insp Aisha, huku ASP ayopub akionekana kukasirishwa na jambo.

Kabla polisi awaanza kuelekea kwenye ofisi za Nyondo, mala wanaliona gari likiondoka toka upande wa pili wa barabara, yani upande wa kituo cha redio, lakini polisi awajari kuhusu gari ilo.***

Naaaaaam, lisaa limoja baadae, makao makuu ya jeshi la polisi, ndani ya chumba kimoja kipana, chenye kuta ngumu, zisizo pitisha sauti toka nje, na utulivu wa kutosha, ungesema ni chumba cha upasuwaji, kwa utulivu wake, lakini hiki ni chumba cha mahojiano.

Ndani ya chumba iki, wanaonekana watu watatu, walio kalia viti vya chuma, vilivyo zunguka meza ya chuma, kwa mpango wa watu wawili, yani Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee, waliokaa upande mmoja wa meza, huku mbele yao kukiwa na vijitabu vidogo vya kunakili, yani note book, na karamu za wino.

Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee wanamtazama kwa macho ya mshangao na kuto kuamini, kijana Hance, alie kuwa katika hali ya utulivu bila wasi wasi, akiwa amevalia tishert jeupe, lenye kulowa damu, mfano wa mfanyakazi wabuchani, mikono yake, ilyofungwa pingu, ikiungwanishwa na myororo, ulio unganishwa kwenye meza nzito ya chuma. lakini alionekana kuwa katika hali ya utulivu, usio na hofu ata kidogo.

“kijana unaitwa nani na una unamiaka mingapi?” anauliza ASP Ayoub Mzee, huku wote wawili wakimtazama kijana, huyu mwenye sura tulivu, ambae uso wake ameutazaisha chini, anatazama mikono iliyofungwa pingu.

“mna uhakika mtasadiki nitakacho waambia?” anauliza Hance au Panya, kwa sauti tulivu, huku bado uso wake ameekeza kwenye mikono, na mkono wake wa kushoto ukiupapasa mkono wakulia.

Insp Aisha na Ayoub Mzee, tazamana kama vile wanakubariana jambo, kisha wanamgeukia kijana mpole, na kuitikia kwa vichwa, kwamba watasadiki kile watakacho ambiwa, “ndiyo tutasadiki” wanasema kwapamoja.

Hance anainua uso wake taratibu, na kuwa tazama maafisa awa awawili, akianza na huyu wakiume, ambae ASP Ayoub Mzee, aliekuwa anachukuwa karamu na kijitabu chake, tayari kuandika atakacho tamka.

Hance anaamisha macho yake kwa afisa Insp Aisha, ambae tayari alikuwa na karamu na kijitabu chake mkononi, akimtazama kijana huyu, ambae amemnusuru toka kibako cha midume mitatu.

“naitwa Panya, namiaka 20” alisema kijana yule, kwa sauti ya taratibu sana, kiuharisia ungetarajia kusikia kicheko toka kwa watu wanao msikiliza, lakini baada yake, chumba kilikuwa tulivu, huku maafisa hawa wawili wakitazamana kwa mshangao. ….ENDELEA….. KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!