
SEHEMU YA TISINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA MOJA: “naitwa Panya, namiaka 20” alisema kijana yule, kwa sauti ya taratibu sana, kiuharisia ungetarajia kusikia kicheko toka kwa watu wanao msikiliza, lakini baada yake, chumba kilikuwa tulivu, huku maafisa hawa wawili wakitazamana kwa mshangao. ….ENDELEA…..
Ni wazi awakulizika na jibu la kijana huyu, alie jitambulisha kwa jina la Panya, ambae ukimtazama hali yake, usinge itaji kuambiwa na mtu kuwa, alikuwa ametoka katika tukio kubwa la umwagaji damu.
Lakini maafisa awa wanakosa namna ya kukataa jina, sababu makubaliano, waliyo yaweka muda mfupi uliopita, yalikuwa ni kwamba, wataamini kile atakachosema.
“ok!, Panya, unaweza kutuambia umepata wapi, umafunzo ya kutumia silaha za aina nyingi, na umewezaje kuuwa watu wengi kiasi hiki, katika umri mdogo kama huo?” aliuliza yule afisa wakike, huku anamtazama kijana huyu mdogo, mwenye jina linalofanana na yule mdudu mdogo mwalibifu.
Lakini kabla kijana huyu ajaongea neno lolote, mala ghafla mlango mzito wa chuma unafunguliwa, kwa pupa, kwa mshtuko mkubwa, maafisa wawili wanageuza nyuso zao na kutazama mlangoni, kwa macho yaliyojaa hofu, wakiamini tayari wamesha vamiwa, na watu ambao wanakuja kumwokoa kijana huyu mdogo, aliejitambulisha kwa jina la Panya.
Hapo wanaonekana watu wanne, huku wawili wakiwa wamevalia suit nyeusi, hao ni mzee Haule, na bwana Mahundi.
Pamoja na RPC alie valia sale za jeshi la polisi, zilizo pambwa na ngao za jeshi la polisi kwenye mabega yake, sambamba na nyota mbili, ikimaanisha ni cheo cha ACP, Asistant Camissioner Polisi, na mwingine akiwa amevalia nguo nadhifu za kiraia, huyu ni RCO Zamoyoni Mpeta.
“sitisha mahojiano, anaitajika kwa mkulugenzi TSA” alisema RPC, kwa sauti iliyojaa amri, na uitaji wa uharaka wautekelezaji, na kuwafanya wakina Insp Aisha wamtazame Hance kwa macho ya mshangao, kabla awaja tazamana na kujiuliza kimoyo moyo “huyu Panya ni nani?”.
Lakini hapa kuwa na mtu wa kuwapatia majibu, hivyo wanamfungua pingu na minyororo, huku Insp Aisha akitamani kumweleza kitu kijana huyu, lakini inakuwa ngumu, maana Hance anatok a mle ndani akiwa na wakina mzee Haule, aya wanapofika nje, wanaingia ndae ndani ya gari, kitu cha kushangaza ni kwamba, ndani ya gari wapo wao tatu tu.
Gari linatoka nje ya uzio wa makao makuu yua jeshi la polisi, wanatembea kuelekea mashariki, lakini awafiki mbali, gari linasimama, “SA-26, au Panya kama mzee Kingumwile anavyopenda kukuita, kuanzia sasa hupo huru, lakini kwa maelekezo mahalumu” alisema mzee Haule, na Hance akatega sikio.
“kwanza kabisa utaendelea kuwa wakara, ila katika kitengo cha ukufunzi, utafundisha mapigano na matumizi ya silaha za jadi” alisema mzee Haule, “Hance anakubari kwa kichwa, “ok!, Farida anakusubiri, ila hakikisha kesho unamrudisha mtoto wawatu chuoni, kumbuka ujamuoa” alisema mzee Haule, nao wakacheka kidogo.
Hance akashuka toka kwenye gari, nalo likaondoka, na wakati huo akiliona BMW likiwashwa mita tachache pembeni kabisa ya barabara, toka pale walipokuwa wamesimama wao, na likamsogelea, nae akaingia nakuondoka zake, akimkuta Farida ndani ya gari, akiwa na lile jacket lake jeusi.***
Naaaaaaam!, siku iliyofuata, yani juma pili saa saba mchana, mateka uhindini, nyumbani kwa bwana Nyondo, watu walikuwa wengi sana, walio onyesha sura za furaha na uchangamfu, huku vilio vikiwa ni vichache sana, watu walijaa upande wa nyuma wa hii nyumba yake kubwa.
Magari na watu mashuhuri na viongozi wa mkoa walikuwepo, mazishi yalikuwa yanakamilika kwamaana makaburi mawili yalikuwa yamesha funikwa, “sipendi kuuwa” aliongea kwa sauti ya chini, Hance aliekuwa amesimama pembeni kidogo ya kundi la watu, akiwa na mwanadada Anastansia, huku nyuma yao mita kadhaa, akiwa amesimama Farida.
“kwahiyo ungewaacha wanichukuwe?” anauliza Anastansia ambae muda wote alikuwa ameshikilia mkono wa Hance, “hapana nisingeweza kuluhusu jambo ilo” anajibu Hance kwa sauti tulivu, ambae leo alikuwa amevaa nguo za kupendeza kidogo.
“we Nancy, hapa unafanya nini, na huyu ni nani unae mshika hivi?” wote wawili wanashtulia na sauti kali ya mwanamke mtu mzima, toka nyuma yao, nao wanageuka kwa haraka na kumtazama.
Naaaaaam!, wanakutana na mama mmoja mtu mzima, ambae licha ya utuuzima wake, lakini alikuwa anavutia kwa mapambo ya usoni, mavazi, aya sura na umbo lake, ni wazi alikuwa ni mke wa kiongozi au yeye mwenyewe anafedha nyingi.
Anastansia anamtazama Hance kwa macho yenye wasi wasi na uoga, “ni mama yangu” anasema Anastansia kwa sauti yenye uoga na kunyongea, huku akisubiri mama yake ata fanya nini baada ya pale.
“Nancy, naona hapa unashindwa kunijibu, ebu ingieni kwenye gari, tukaongee mbele” alisema mama Nancy, huku anamshika mkono Anastansia, na kumwongoza kwenye maegesho ya magari.
“lakini mama….” anasema Anastansia lakini, mama yake anamuwai, “sitaki uniambie chochote, twendeni nyumbani tukaoongee, yani Nancy unashindwa ata kumnunulia rafiki yako nguo nzuri, ona anavyo onekana kijana mzuri, lakini utasema ametoka shammba” anasema mama Anastansia, huku anaendelea kuwaongoza vijana awa kuelekea kwenye gari lake.
Lakini ilo alikuwa tatizo kubwa, kwamaana baada ya mama Anastansia kusimuliwa kilicho tokea siku mbili zilizopita, na kufafanuliwa kila kitu, hakika alibariki mausiano hayo ya binti yake, na kuwataka wafunge ndoa mapema baada ya Nancy kumaliza chuo mwaka unaofwata.
NAAAAAAAAAAAAM HUO NDIO MWISHO WA HADITHI HII FUPI, YA #TOBO_LA_PANYA, ASANTE KWA KUWA NA MIMI MWANZO MPAKA MWISHO KAA TAYARI KWA HADITHI NYINGINE YA MOTO. HAPA HAPA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU