UTAMU WA JAMILA (14)

SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA
Alimrushia funguo kisha akatoka zake nje kuelekea kazini kwake huku mwenzake akionesha kuchukia sana.

SONGA NAYO
Hadi jioni inafika kila mtu alikuwa ametosheka na huduma ya mwenzake. Badu alikuwa akimalizia kuvaa shati lake vema huku Jesca akiwa kitandani amekaa anajipaka mafuta mwilini.
“Yani nikifika nyumbani ni kulala tu kwakweli maana umenipinda haswaa. Sijawahi fanya matusi kiasi hiki jamani kaah!”aliongea Jesca na maneno yake yalimfanya Badu acheke tu.

Kicheko chake kilimfanya Jesca aachie tabasamu huku akionesha kweli kuchoka.
” Haya bwana, uniambie lini tutarudia tena?”aliuliza Badu kwa makusudi.

“We koma, hapa sina hamu kabisa Badu kwa jinsi tulivyoshinda tunafanya tu hadi muda huu sijui kama nitakutana na mtu kwasasa.” aliongea Jesca alivaa nguo zake.

“Halafu umenikumbusha hivi muda ule ulivyonambia nikufowadie ile meseji ulontumia ulikuwa wapi?”aliuliza Badu na kufanya Jesca acheke.

“Ah kuna boya mmoja hivi nilikuwa naye, tena alitaka twende Bagamoyo tukakae huko siku mbili sema ah hana maajabu nikaona atanichosha tu ndio maana nikakuambia vile. Yaani nilikupania wewe tu sio siri na sijui umenifanya nini maana sijielewi ujue.”

“Ah sasa hujielewi nini Jesca?”

“Nashangaa ujue sijawahi kugawa tamu yangu bure tu kwa mtu. Mimi na watu wakubwa wenye pesa zao ndio type yangu tu kama huyu niliyemtoroka. Ila nashangaa sijui imekuwaje umeniteka nakupa tena na tena hadi najishangaa.”alisema Jesca akiwa anamtazama Badu.
Alitabasamu tu mwenyewe na kusogea taratibu pale kitandani kisha akambusu Jesca shingoni.

” Wala sijakufanya kitu Jesca ni mapenzi tu hayahaya unayoyaona kitandani hakuna kingine.”

“Mmh haya bwana, ila nikwambie tu ukweli Badu. Yaani wewe unajua tena na tena, yaani mwili wangu umeutendea haki ipasavyo.”

“Mh haya asante dear. Kwahiyo nianze kujiandaa na hela sasa nikitaka mchezo kwako.”

“Ah wapi! Hapa wewe ni staff nakupa ofa mpaka nizikwe.” alisema Jesca na kumfanya Badu afurahi kusikia hivyo. Alimpa busu la motomoto, naye Jesca alipokea na kujikuta wanaganda hivyo zaidi ya dakika nzima, kisha akamshika mkono kumnyanyua.

“Tuondoke sasa kama tayari ushavaa.”aliongea Badu akimuangalia Jesca usoni akiwa amelegea macho.

” Sawa my.”

Walitoka pamoja ndani ya chumba hicho huku nje giza likianza kushika nafasi yake. Ilisogea bodaboda pale wakapanda kurudi kwao moja kwa moja.

Hadi muda huo Roja hakuwa na dalili za kurejea kwake kabisa huku dhahiri shahiri akionekana kutingwa na kazi ya kutengeneza gari.
Hali hiyo ilizidi kumtibua Mwajuma ambaye muda wote alikuwa tu mule ndani akimsubiri mpenzi wake huyo. Muda mfupi ujumbe uliingia kwa Mwaju na kupata kuona ni Roja ambaye ameutuma ikabidi asome.

“My naomba nisamehe kwakweli hii kazi sio ya kitoto. Hapa natoka na tajiri twende mjini kuna kifaa tunaenda kuchukua. Naomba rudi home kwaleo my kesho njoo.”

Ujumbe huo ulimfanya Mwajuma atoe sonyo kubwa huku akinyanyuka kutoka kitandani ambako alikuwa amejilaza anachezea simu. Alivaa nguo zake kuvaa, na kwa hasira alichukua beseni kubwa lililo pembeni kisha akachukua nguo safi zilizo kabatini akaziweka humo. Alichukua maji akajaza kisha akazishindilia na mguu, yote tu ni kwa hasira za kuwekwa muda wote huo bila kupata kile ambacho anahitaji. Alitoka na kufunga mlango kisha akaitupa funguo pale mlangoni na kumtumia ujumbe Roja. Akazima simu yake na kuchukua bodaboda kurudi kwao.

Muda wote huo mama mwenye nyumba alikuwa zake ndani akiwauliza wapangaji kuhusu binti yake Mwajuma kama ameaga alipotoka. Hakuna aliyefahamu kuhusu mwanaye, akirejea zake ndani na kuendelea kupika. Alinyanyua simu yake kumpigia lakini namba ya Mwajuma haikuwa hewani muda huo.

“Huyu pimbi kaenda kuzululia wapi tena? Yaani nimetoka na baba yake naye huku katoka kaacha nyumba pekeake.”alilalama mama J akiwa anageuza mboga zake jikoni.

Muda mfupi tu Jesca aliwasili nyumbani hapo ambapo baada ya kufungua geti moja kwa moja alielekea zake chumbani kwake. Aliwakuta baadhi ya wapangaji wamekaa wamekaa nje kila mtu akiwa anapika nje ya mlango wa chumba chake, aliwasalimia na kuingia zake ndani.

“Mama Dula, hivi huyu msichana anafanyaga kazi gani maana namuonaga onaga tu ujue!”aliuliza mama mmoja aliyekuja kumtembelea shoga yake.

” Ah miye sifuatiliagi maisha ya mtu. Ila sijawahi kumuonaga anaenda kazini zaidi ya kuingiza mabwana tu.”

“Ehee hapo sasa nimekuelewa. Unajua sikuwahi kukwambiaga kitu ila uwe na kaba usije kuyavuruga mambo hapa.”

“Mh we nayee! Haya niambie kuna ubuyu gani tena?”aliuliza mama Dula akiwa anaepua mboga yake na kubandika maji ya ugali.

“Mwenzangu kuwa makini naye huyu msichana. Nasikia yeye anaangalia mfuko tu wa mwanaume, na hajali huyu ni mume wa mtu ama nani yeye anabeba tu.” alisema mwanamama huyo mgeni.

“Mh we mama Rama hebu acha bwana. Umeyatoa wapi hayo?”

“Eehee ndio nakwambia sasa uwe makini na wewe.”

“Makini kivipi tena mbona wanichanganya!’

“Acha kujifanya hujui mfunge kamba mumeo shauri yako.”

“Ahahaha! Haloooo hebu niache miye nimpikie laazizi wangu ugali miye. Hayo mambo abadani hawezi kufanya baba Dula. Namuamini na ananiamini hawezi kwenda kutembea na vitoto vidogo hivi.”

“Mh haya mimi nimekueleza tu.”

“Bwana wewe hanishtui kabisaa huyu msichana wala usiwe na hofu. Vipi kwanza vijora umeenda kuchukua mjini?” alihoji mama Dula na stori zengine zikaendelea baada ya kupuuzia yale aloambiwa.

Muda mfupi Mwajuma aliingia humo na moja kwa moja akaingia zake kwao bila kusalimia mtu nje. Hata alipofika ndani alipata kumuona mama yake jikoni anapika.

“Haya bibi wewe umetoka wapi?”aliuliza mama huyo.

“Ah mama niache nipumzike sitaki kusimbuliwa.”alisema Mwajuma na kuingia zake chumbani kwake akionekana kutokuwa na furaha kabisa. Mama mtu alibaki kushangaa tu asijue kimemkuta nini mwanaye

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!