UTAMU WA JAMILA (26)

SEHEMU YA 26

Iliwachukua nusu saa kumaliza jambobl lao ambalo wao waliamini ni siri yao wakiwa ndani. Mama J aliinuka na kupandisha chupi yake akavaa dela lake na kuelekea zake mlango wa nje. Alishangaa kuona upo wazi kabisa angali aliufunga baada ya kijana yule kuingia. Alibaki kuutazama vema ule mlango huku akivuta kumbukumba kama kweli aliufunga ama laa!

“Ah bwana eh!” hakuonesha kujali kabisa alitoa kichwa nje kuangalia hali halisi. Alipoona kumetulia akarejra tena ndani kwenda kumtoa yule kijana ambaye alipotoka moja kwa moja akaondoka zake.
Na muda huohuo Jesca aliweza kutoka nje akiwa na tabasamu murua kabisa, bila kupepesa alikodoa macho kule alipo mama J ambaye naye alikuwa anamtazama mpangaji huyo akitoka. Wakabaki wanatazama kwa muda huku Jesca akiamua kukaa kabisa kibarazani kwake pale na kuanza kubofya simu yake hana habari.

“Mh huyu ameniona au? Mbona ananiangalia vile?” aliongea Mama J kisha akageuka kuingia zake ndani kwake.

Hakuwa na amani tena kila akikumbuka jicho la Jesca vile alivyokuwa akimuangalia na kuhisi kuna kitu hapa kati.

“Hapana huyu malaya kama amejua atakuja kunisambazia hata kwa mume wangu ikawa kesi sasa. Ah nifanye nini hapa! Niende kumdadisi au inakuwaje? Lakini nisije kujipeleka kuropoka kumbe yeye hana analojua! Ah sasa nifanyeje!” Alishindwa kuelewa nini atafanya kwa mpangaji wake.
Hakutaka kuumiza sana kichwa chake kwa swala hilo aliamua kuendelea na kazi zake.

Baada ya muda kidogo alipata kuingia ndani mama mmoja na moja kwa moja akaelekea zake chumba cha mama Dula kumgongea mlangoni. Ulifunguliwa na kuonekaka mama huyo akiwa mwenye tabasamu.

“Karibu shogangu.”

“Asante mlilala nini nimekuja kuwasumbua.”

“Ah wala tulikuwa tunaangakia tamthilia tu kwenye Tv na mwanangu.”aliongea mama huyo akiwa amesimama kwenye mlango wake.

“Haya mwaya, vipi mzee yupo ndani?”

“Mh saahizi huwezi mkuta kashaenda kwenye minara yake huko. Vipi unashida naye?”

“Akaa miye mume wa mtu wa nini bibiwee.”aliongea mama huyo na wote wakaanza kucheka.
“Mama Dula. Unakumbuka majuzi nilikuja hapa nikakwambia swala la kumfunga kamba mumeo? Unakumbuka.”
“Mh nakumbuka ndio, amefanyaje mumewangu?”
“Mh mwenzangu za kusikia sikia ni huyu mama mwenye nyumba yenu safari hii.”
“Mh wewe mbona sikuelewo, imekuwaje? Mama mwenye nyumba kafanyeje?”aliuliza mama Dula huku akitoka nje vizuri na kuufunga mlango.
” Nimesikia jana mumeo alionekana mtaa wa tatu huko akitoka gesti na huyu mama mwenye nyumba.”aliongea mama huyo huku akimtazama mwenzake.
Alishangaa kumuona mama Dula anaanza kubadilika kama mwenye presha.
“Mmmmmm nini sasa! Umeshaanza nitakuwa sikuletei habari nazosikia huko maana unajitia kama unakichaa.”
” Mama Ally hebu… Ah unachosema ni kweli au?”
“Mimi nimesikia kwa watu ambao nawaamini. Na kama unakumbuka niliwahi kukwambia muangalie mumeo japo ilikuwa kwa yule binti. Nawe ukasema unamuamini baba Dula sasa kikowapi! Ameenda gesti na mwenye nyumba kimya kimya wamefanya mambo yao. Wewe unajua mtu yupo kazini kumbe anapewa uroda na huyu mama malaya.”
“Basi, basi mama wewe nenda nitajua nini nitafanya. Usiku mwema.”aliongea mama Dulla na kuanza kuingia ndani.
“Basi ndio usinitaje huko nikaja kusutwa bure. Nimekueleza najua mwenzangu unakaba usiniangushe.”aliongea mama Ally na kumuona akiitikiwa kwa kutikisa kivhwa mama Dulla kisha akaufunga mlango wake.
“Mh makubwa!”aligeuka zake mama Ally baada ya kuleta taarifa hiyo kisha akaanza mwendo.

Hakuweza kabisa kurudi tena sebuleni kuendelea kuangalia tamthilia. Taarifa hiyo kwake ilikuwa nzito sana na hakuwahi kufikiria kabisa kama kuna siku anaweza akapokea kesi kuhusu mumewe. Alimuamini sana ndio maana alijiamini kila anapokuwa na kumtetea mumewe kwa mambo mabaya yakuhisiwa. Lakini habari hiyo ya sasa kumhusu mama mwenye nyumba na mumewe ilimgusa sana na kuhisi huenda linaweza kuwa kweli.
“Hapa nisipoangalia naweza kuletewa magonjwa humu ndani bila kujijua.”alisema Mama Dulla akiwa zake kitandani ameshika shavu kwa kutafakari.
Alinyanyua simu yake kutafuta namba ya baba Dulla. Aliitazama namba hiyo akijiuliza aanze kumpigia muda huohuo au apoe kwanza. Punde tu aliingia mwanaye chumbani akiwa analia kutaka aogeshwe. Ilibidi aache simu pale kitandani kwenda kumuogesha mtoto kwanza.

Mishale ya saa tatu kuelekea na nusu usiku Badu na Mwajuma walikuwa wanaingia baada ya kukimbia sana siku hiyo. Kila mtu alikuwa amelowa chapachapa kwa jasho. Waliagana na Mwajuma akaingiza kwao huku Badu akifungua mlango wake kuingia chumbani kwake. Siku hiyo alichoka haswa hivyo alielekea zake bafuni kuoga mapema na baada ya muda akarudi kuufunga mlango akiwa hataki kabisa kusumbuliwa na mtu.
Aliendelea kuperuzi akiwa kitandani na daika chache tu simu yake ilipata kuita, alipotazama aliona jina la BOSS, aliachia tabasamu na kupokea haraka
” Ndio boss habari yako.”
“Safi Badu vipi umeshalala?”
“Hapana boss bado sijalala.”
“Sawa, kwanza pole kwa kukaa nyumbani kwa miezi kadhaa kutokana na ishu ile ilotokea. Pia nisamehe bwana nimepata kuujua ukweli kumbe haukuwa wewe mwenye hatia. Bahati ndiye aliyechukua pesa zile na alitubu mwenyewe kuwa kweli. Sasa kesho mapema naomba uanze kazi. Nategeme kukuona asubuhi kazini.”
“Dah aisee bosi nashkuru sana kwa kunirejesha tena maana mtaani hakuna ishu kabisa. Mimi kesho nitawasiki mapema sana.”
“Haya sawa nikutakie usiku mwema.”
“Na kwako pia bosi.”alijibu Badu akionesha kufurahishwa sana.
Alishusha pumzi baada ya kumaliza kuwasiliana na bosi wake. Haraka akanyanyuka kutoka kitandani kuelekea kwenye kabati lake. Alifungua na kuangalia nguo. Alitoa shati jeupe la mikono mirefu lililokuwa na nembo ya hoteli moja mashuhuri pamoja na suruali nyeusi. Aliziweka sawa akijua kesho anarudi zake kazi baada ya muda mrefu kukaa nyumbani bila kazi…..  

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!