
SEHEMU YA 50
Asubuhi ya saa tatu Jesca ndio aliweza kuiona ile sms ya Badu baada ya kuwasha simu. Alishangaa sana kwa uamuzi huo aliouchukua Badu. Aliamua kutoka akamuulize imekuwaje hadi kuamua hivyo.
Alipotoka alimkuta Badu na mzee Chombo wakiwa wamesimama wakiongea. Ilimbidi atulie kwanza kuwasubiri wamalize.
“Lakini kwanini unataka kuhama na bado mapema sana kijana?”aliuliza mzee Chombo wakiwa wamesimama na Badu nje ya chumba chake.
“Hapana mzee nimeamua tu nibadilishe mazingira. Na tayari asubuhi hii nimeshapata chumba huko nilipokwenda kutafuta.”alisema Badu na kumuona mzee huyo akitabasamu.
“Nilipata kusikia taarifa zako kijana japo sijathibitisha kama zinaukweli wowote. Kama umeamua kuhama kwaajili hiyo basi sawa na nitajiaminisha kuwa kweli ulikuwa unatembea na mabinti za watu. Umechukua uamuzi sahihi, vema ukaondoka tu ili usizidi kuchafuliwa jina lako au siku ukakamatwa kijana wangu, maana hakuna mzazi atakayekubali kuona binti yake anaharibiwa na mtu.”alisema mzee huyo na kumfanya Badu apoe tu bila kusema lolote.
Baadae mzee huyo aliondoka zake akimuacha Badu akiwa amesimama pale, aliamua kuingia zake ndani tu baada ya kumueleza mzee huyo.
“Badu.”aliita Jesca akimsimamisha kijana huyo kuingia ndani.
“Nini kimetokea kwani? Meseji yako sijaielewa, unataka kuhama?”
“Ndio nimeamua tu kufanya hivyo?”
“Jamani kwanini sasa?”
“Jesca, moyo wangu tu umeamua kufanya hivyo. Sasa nataka nianze maisha yangu mapya yasiwe na haya maigizo ya mapenzi ndani yake.”
“Lakini Badu si tayari nimeshajua kuwa unamahusiano na Mwajuma. Mimi nimeridhika niwe wa ziada na naenjoy tu, sasa nini tatizo!”alihoji Jesca akiwa anamtazama Badu usoni.
“Nisikilize Jesca, haya maisha kwangu mimi nimeyachoka. Sasa nataka niwe na mmoja tu nianze naye maisha. Sitaki niyaingilie maisha yako ambayo yanakuweka mjini. Endelea nayo kama waona ndio kila kitu kwako japo naweza kukushauri uachane nayo, tafuta kazi ya maana ufanye. Maamuzi yangu ndio hayo mpendwa.”alisema Badu akionekana kweli kushikilia msimamo wako.
Alimfanya Jesca ashushu pumzi htku akitazama chini, muda huohuo geti lilipata kufunguliwa na kupata kuonekana baba Dula akiwa na begi akiingia pamoja na mkewe. Moja kwa moja walielekea chumbani kwao wakapata kujifungia ndani. Ni wazi ugomvi wao umesuluhishwa mara baada ya baada Dula kukubali kosa lake na kukiri mbele ya wazazi wa pande mbili kuwa amebadilika kuwa mpya sasa.
Ilimuaminisha mama huyo kuona kweli mumewe amekubali kosa na kuomba samahani.
“Mke wangu, nashukuru kwa kurejea tena na kuwa upande wangu, ila nahitaji hapa tuhame. Nitatafuta mahala pengine pa kuishi ili niepuke na hivi vishawishi vinavyoendelea humu ndani.”aliongea baba Dula akiwa anamaanisha.
“Hilo ndio lilikuwa pia akilini mwangu. Kweli nimeamini umekuwa bora kwangu sasa mumewangu.”alisema mama Dula na wote wakaachia tabasamu na kukumbatiana kwa furaha.
Huku nje bado Jesca alikuwa akitafakari uamuzi wa Badu wakiwa wamesimama pale.
“Sio siri Badu umeshaniharibu kinamna fulani yaani ipite siku bila kukuona, ipite wiki usinifanye kwakweli sitaweza. Wewe nenda huko unapokwenda ila uwe unakuja kwangu kunipa raha tu. Siku yoyote ile unayotaka hata nikiwa wapi nitarudi kwaajili yako. Na kama ukishindwa basi nitakuja mimi kwako. Naomba uniruhusu hilo tu!”aliongea Jesca akiwa mwenye kutia huruma kweli. Hakika aliona kulikosa penzi la Badu kwake itamuumiza sana.
“Sidhani kama nitaweza hilo swala Jesca, utanisamehe.”aliongea Badu kisha akaingia zake ndani.
Mwili aliuona mzito Jesca haamini kile alichoambiwa. Kwa unyonge aligeuka na kurudi zake chumbani kwake.
Mzee Cholo alimfikishia taarifa hiyo mkewe, taarifa ambayo ilimshtua sana.
“Kwahiyo umemfukuza wewe au?”aliuliza mama huyo akiwa anakunja nguo zake chumbani.
“Wala ni yeye mwenyewe kaniita ndio kaniambia kuwa huenda leo au kesho akahama. Nadhani kile ulichokitaka mkewangu kimetimia, na inaonesha kweli kijana alikuwa na matendo hayo maana ni gafla tu kuchukua uamuzi huo.”aliongea mzee Chombo akichukua gazeti lake akatoka kuelekea sebuleni.
Mama J alishindwa kuamini jambo hilo, ni kweli yeye ndio alitaka Badu atolewe humo baada ya kujua kuwa binti yake pia anamahusiano na kijana huyo. Lakini moyo wake umebadilika gafla tena baada ya kupewa raha siku chache tu huku akiamua kuendelea kuchepuka kwa kijana huyo tu.
“Haiwezekani huyu kijana ameshayapandisha maruhani yangu tena ndio anataka kuondoka. Hapana kwakweli.”aliongea mama huyo akiwa hataki kukubali jambo hilo litokee kwa Badu kuhama.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU