
LOML | Love Of My Life (187)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:187
Dawa hazikuwa zinamsaidia kabisa mtoto wangu, alizidi kuwa na hali mbaya sana. Hali yake ilikuwa mbaya mno, mno kwa mtoto wangu.
Ilinibidi nirudi hospitali, walimfanyia vipimo mtoto wangu, lakini hakuwa anaonekana ana tatizo. Mimi nilikuwa nalia hata namuuliza dokta βkwani dokta mtoto wangu ana shida gani?β
Dokta huyu alinitazama, na kuniuliza βmtoto anaitwa nani vile?β
Nilimtajia jina lake, alinitazama na kusema βhuyu si wakiume?β
Nilimwambia kwa upole nikilia βndiyo ni wa kiume.β
Aliniambia βhili jina mbona maana yake sio nzuri kwa mtoto wa kiume.β
Nikauliza kwa upole βmaana yake nini dokta?β
Huyu dokta aliniambia βni nani aliyempa jina hili?β
Nikainamisha tu kichwa, basi huyu dokta alinaimbia βhuko kwetu maana yake ni mwanamke asiyeambilika.β
Nikashtuka na kusema βmwanamke asiyeambilika, Mungu wangu!!β
Huyu dokta alinitazama na kusema βsikia unaweza kusema mtoto anaumwa kumbe unatakiwa kuomba, mimi sijui sana. Chukua namba hii ya huyu mtu atakusaidia sana. Atakusaidia kwenye maombi yupo vizuri.β
Nilikuwa nashangaa tu, alinitazama na akaniuliza βna vipi macho?β
Nikamwambia tu βnimepata dawa dokta.β
Nilimshukuru sana na kuondoka nikiwa na hasira. Nilifika nyumbani mwanangu analia mpaka nachanganyikiwa. Nilimpigia bibi yangu simu nikamuelezea kila kitu.