
LOML | Love Of My Life (197)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:197
Nilivuta pumzi na kisha niliendelea โMama babuu, jitahidi sana kwenye hilo. Nataka amani zaidi kuliko chochote kile. Kabla Sijasahau huyu mwanamke mzuri mbele yako unayemuona anaitwa Pina.
Huyu ndiyo mpenzi wa maisha yangu na huyu sasa ndiyo Madam wako. Yupo huru hapa muda wowote na wakati yoyote akiwa hapa tafadhali fanya kila anachokuelekeza. Anaitwa Pina.โ
Mama babuu alitabasamu na kusema โnashukuru sana kukufahamu madam.โ
Pina alitabasamu, na kisha niliendelea โPina anaitwa mama Babuu, ni mama yangu hapa nyumbani. Mama mzuri sana tafadhali nategemea mtaishi kwa upendo.โ
Pina alitabasamu na kuniambia โasante sana mpenzi, nimefurahi kukufahamu mama. Mimi naitwa Pina.โ
Wakapeana Mikono na wakati huo Pina alikuwa anatabasamu tu. Na mama Babuu alinionesha kidole gumba cha safi sana akionekana kuwa na furaha sana. Nilitabasamu nikisema โmama Babuuu, unaweza kuendelea na mambo yako sasa.โ
Mama Babuu akawa anaondoka, hakufika mbali nilisema โmama Babuuu, naomba msaidiane na mlinzi tafadhali. Kule chumbani kitu chochote cha Gabby naomba kitoke. Na hata hivyo vitu vyangu hamishia chumba kingine, na kile kitanda kiondoke kabisa nitaagiza kingine sitaki kiwepo hapa nyumbani.โ
Mama babuu alinitazama na kuniuliza โina maana kitanda?โ
Nikamuuliza โuna kihitaji?โ
Aliinamisha kichwa chini, na kisha nikaendelea โkitanda ni sehemu nzuri sana. Kama una hitaji siwezi kukukatalia. Ila tayari hiko kitanda kina roho kimebeba kama unaweza jitenganisha na roho hizo kichukue haina shida.โ
Mama Babuu alitabasamu na kufurahia sana. Halafu Mimi nilimuongoza Pina aliketi.

