
LOML | Love Of My Life (187)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:187
Dawa hazikuwa zinamsaidia kabisa mtoto wangu, alizidi kuwa na hali mbaya sana. Hali yake ilikuwa mbaya mno, mno kwa mtoto wangu.
Ilinibidi nirudi hospitali, walimfanyia vipimo mtoto wangu, lakini hakuwa anaonekana ana tatizo. Mimi nilikuwa nalia hata namuuliza dokta โkwani dokta mtoto wangu ana shida gani?โ
Dokta huyu alinitazama, na kuniuliza โmtoto anaitwa nani vile?โ
Nilimtajia jina lake, alinitazama na kusema โhuyu si wakiume?โ
Nilimwambia kwa upole nikilia โndiyo ni wa kiume.โ
Aliniambia โhili jina mbona maana yake sio nzuri kwa mtoto wa kiume.โ
Nikauliza kwa upole โmaana yake nini dokta?โ
Huyu dokta aliniambia โni nani aliyempa jina hili?โ
Nikainamisha tu kichwa, basi huyu dokta alinaimbia โhuko kwetu maana yake ni mwanamke asiyeambilika.โ
Nikashtuka na kusema โmwanamke asiyeambilika, Mungu wangu!!โ
Huyu dokta alinitazama na kusema โsikia unaweza kusema mtoto anaumwa kumbe unatakiwa kuomba, mimi sijui sana. Chukua namba hii ya huyu mtu atakusaidia sana. Atakusaidia kwenye maombi yupo vizuri.โ
Nilikuwa nashangaa tu, alinitazama na akaniuliza โna vipi macho?โ
Nikamwambia tu โnimepata dawa dokta.โ
Nilimshukuru sana na kuondoka nikiwa na hasira. Nilifika nyumbani mwanangu analia mpaka nachanganyikiwa. Nilimpigia bibi yangu simu nikamuelezea kila kitu.

