
LOML | Love Of My Life (170)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:170
Wote watatu tulicheka. Kisha Willy alinitazama na kusema “tumpigie Dereva amuwahishe Pina, na kisha mimi nikaangalie mishe si unajua eenh. Kisha baadaye narudi hapa.”
Nikamwambia “mpigie basi wakati tunamsubiri unatoa maelekezo.”
Tuliendelea kucheka na kisha aliniambia “amesema anakuja tusubiri kaka.”
Basi ndiyo akawa ananiambia kuwa walikuwa wakinitafuta na bahati mbaya kazini niliwaelekeza kuwa unaumwa hivyo walifika kazini wakaambiwa mimi nimesema hivyo. Basi mama akanitafuta mimi na sikuona sababu ya kuendelea mficha na kumbe mkeo na yeye anakutafuta wakiwa wote.
Nilitabasamu nikisema “Gabby!!, Gabby!!, Gabby!! Na vipi baba. Simu yangu iko wapi?”
Willy alinisaidia kutazama simu na akasema “ina missed calls kama zote.”
Kutazama nilisema “Mungu wangu sikuweka sauti kabisa. Na baba amejua kunitafuta.”
Pina aliniambia kwa upole “mtoe hofu.”
Basi niliendelea kukagua simu yangu, naona kabisa Gabriella eti amepost status yake hana aibu kabisa “Get well soon hubby, ukiumwa naumwa. Nakupenda sana.”
Tena amechagua picha yangu nzuri kweli, hana aibu hata. Nilitazama na kukasirika, nilimblock kabisa, maana naona anachanganyikiwa vibaya sana.
Pina na Willy waliamua kuniacha tu, ulipita muda mimi nahangaika na simu Willy alisema “dereva amefika sasa.”
Pina alisimama na kusema “nitarudi kwaajili yako Ricky.”
Nilitabasamu na kusema “baby Please, know that i love you na nakusubiri hapa.”
Pina alitabasamu na kujibu “anything for you handsome!!”

