LOML | Love Of My Life (187)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:187

Dawa hazikuwa zinamsaidia kabisa mtoto wangu, alizidi kuwa na hali mbaya sana. Hali yake ilikuwa mbaya mno, mno kwa mtoto wangu.

Ilinibidi nirudi hospitali, walimfanyia vipimo mtoto wangu, lakini hakuwa anaonekana ana tatizo. Mimi nilikuwa nalia hata namuuliza dokta “kwani dokta mtoto wangu ana shida gani?”

Dokta huyu alinitazama, na kuniuliza “mtoto anaitwa nani vile?”
Nilimtajia jina lake, alinitazama na kusema “huyu si wakiume?”
Nilimwambia kwa upole nikilia “ndiyo ni wa kiume.”

Aliniambia “hili jina mbona maana yake sio nzuri kwa mtoto wa kiume.”
Nikauliza kwa upole “maana yake nini dokta?”
Huyu dokta aliniambia “ni nani aliyempa jina hili?”

Nikainamisha tu kichwa, basi huyu dokta alinaimbia “huko kwetu maana yake ni mwanamke asiyeambilika.”
Nikashtuka na kusema “mwanamke asiyeambilika, Mungu wangu!!”

Huyu dokta alinitazama na kusema “sikia unaweza kusema mtoto anaumwa kumbe unatakiwa kuomba, mimi sijui sana. Chukua namba hii ya huyu mtu atakusaidia sana. Atakusaidia kwenye maombi yupo vizuri.”

Nilikuwa nashangaa tu, alinitazama na akaniuliza “na vipi macho?”
Nikamwambia tu “nimepata dawa dokta.”

Nilimshukuru sana na kuondoka nikiwa na hasira. Nilifika nyumbani mwanangu analia mpaka nachanganyikiwa. Nilimpigia bibi yangu simu nikamuelezea kila kitu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata