
LOML | Love Of My Life (197)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:197
Nilivuta pumzi na kisha niliendelea “Mama babuu, jitahidi sana kwenye hilo. Nataka amani zaidi kuliko chochote kile. Kabla Sijasahau huyu mwanamke mzuri mbele yako unayemuona anaitwa Pina.
Huyu ndiyo mpenzi wa maisha yangu na huyu sasa ndiyo Madam wako. Yupo huru hapa muda wowote na wakati yoyote akiwa hapa tafadhali fanya kila anachokuelekeza. Anaitwa Pina.”
Mama babuu alitabasamu na kusema “nashukuru sana kukufahamu madam.”
Pina alitabasamu, na kisha niliendelea “Pina anaitwa mama Babuu, ni mama yangu hapa nyumbani. Mama mzuri sana tafadhali nategemea mtaishi kwa upendo.”
Pina alitabasamu na kuniambia “asante sana mpenzi, nimefurahi kukufahamu mama. Mimi naitwa Pina.”
Wakapeana Mikono na wakati huo Pina alikuwa anatabasamu tu. Na mama Babuu alinionesha kidole gumba cha safi sana akionekana kuwa na furaha sana. Nilitabasamu nikisema “mama Babuuu, unaweza kuendelea na mambo yako sasa.”
Mama Babuu akawa anaondoka, hakufika mbali nilisema “mama Babuuu, naomba msaidiane na mlinzi tafadhali. Kule chumbani kitu chochote cha Gabby naomba kitoke. Na hata hivyo vitu vyangu hamishia chumba kingine, na kile kitanda kiondoke kabisa nitaagiza kingine sitaki kiwepo hapa nyumbani.”
Mama babuu alinitazama na kuniuliza “ina maana kitanda?”
Nikamuuliza “una kihitaji?”
Aliinamisha kichwa chini, na kisha nikaendelea “kitanda ni sehemu nzuri sana. Kama una hitaji siwezi kukukatalia. Ila tayari hiko kitanda kina roho kimebeba kama unaweza jitenganisha na roho hizo kichukue haina shida.”
Mama Babuu alitabasamu na kufurahia sana. Halafu Mimi nilimuongoza Pina aliketi.

