SEASON 01: LOML | Love Of My Life (01)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:01

Leo nataka niwape hadithi ya maisha yangu, hadithi ambayo mtanitumia mimi kama mfano na kuishi mazuri yangu na kuachana na mabaya yangu ambayo nitakuwa nimeyafanya katika maisha yangu.

Jina langu ni Rodrick, mimi naitwa Rodrick. Sitaki kukuzungusha sana, nitaenda moja kwa moja na mengine tutajua hapahapa nitajitahidi sana uelewe kila kitu.

Nataka tu nianzie pale maisha yangu yalipoanza kuonesha upande wa pili wa dunia yangu. Na hapa ndiyo niliamini kuwa hakuna kitu hutokea bahati mbaya kwa maisha ya mwanadamu, kila kitu kina sababu, iwe nzuri au mbaya lakini tayari ni sababu na sababu hiyo itakupeleka mahali. Na hii ndiyo ilinitokea na mimi.

Mimi kwenye maisha yangu ninaye mchumba ambaye sasa nalazimika kumuoa kwasababu ana mimba yangu. Ninampenda, ndiyo nilikuwa naona hivyo, lakini kumuoa sikuwa tayari lakini familia yangu, na familia ya mpenzi wangu Gabriela zilikuwa zinasisitiza sana juu ya ndoa yetu kwasababu ya hadhi na heshima zao watawezaje kuficha hili hivyo ni lazima tuoane.

Hata yeye mwenyewe mpenzi wangu G, aliniambia kwa kudeka β€œeenh Rodrick, sasa mpenzi, nina mimba, tuoane au hunipendi babe eenh, niambie nijue.”
Nilimtazama na kusema kwa upole β€œG unajua sana kuwa mimi nakupenda unajua hilo, lakini kuhusu kuoa nilikuwa bado.”

G alinitazama na kusema β€œhofu yako ni nini sasa, tuna kila kitu Ricky, kila kitu tunacho sasa sijui unataka nini?, au mwenzangu hunipendi kama ninavyokupenda, kama hunipendi niambie, tell me.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

LOML | Love Of My Life FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

KIBOKO YANGU FULL