LOML | Love Of My Life (02)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:02
Nilimtazama tu, sasa huyu ndiyo mpenzi wangu G. Ni mwanamke ambaye sio mvumilivu, ana pesa mbele sio mambo mengine, anapenda anachotaka muda na wakati huohuo kifanyike na kiwe. Ni binti mzuri sana ila ana mambo mengi ambayo mimi kama mwanaume naona kabisa kwa ndoa inakuwa ni ngumu sana hivyo nilihitaji muda zaidi.

Nilimshika mkono, na kusema β€œbaby wangu G, wala hata sio hivyo. Nina hofu tu, nina ogopa sana sijui hata itakuaje. Lakini ukweli ni kwamba natamani kukuoa hata sasa hivi, hofu tu.”

Gabriella alinitazama na kutabasamu akisema β€œmpenzi unaenda kuwa baba, hili ni jambo zuri sana kwetu, unaenda kuwa baba fanya kwaajili yetu. Tutafurahi sana.”

Nilitabasamu tu, sikuwa na la kufanya mimi. Kila mmoja alikuwa anasubiri ndoa yangu kasoro mimi hapa, mimi peke yangu ndiyo nilikuwa natamani ndoa isiwe. Ningefanya nini mimi, zaidi ni kukubaliana na ukweli kuwa natakiwa kumuoa Gabriella mchumba wangu wa muda mrefu.

Kila kitu kilikuwa sawa kabisa, maandalizi, familia, mavazi, ukumbi, kila kitu kilikuwa ni sawa kabisa. Mpaka wasimamizi wa ndoa yetu walikuwa wapo pale. Na kila mtu alikuwa anafurahia siku hii. Siku ilifika sasa, mimi na Gabriella kufunga ndoa yetu takatifu kabisa. Watu walifurahi, hakika ilikuwa harusi nzuri sana, ya kisasa na yenye furaha sana. Sijui nikuambie nini kila kitu kilikuwa safi kabisa.

Kama ungepata nafasi ya kumuona Gabriella sasa, ni kama vile anatamani dunia yote ingekuwa inajua kuwa yeye leo anafunga ndoa. Alikuwa amechangamka, ana furahia sana, amecharuka nakuambia simu anapost, anaandika kile anataka unajua vile ilivyo kwa mtu ambaye ametamani kitu kwa muda mrefu sana na sasa amekipata, ndiyo ilivyokuwa kwa Gabriella, alifurahi sana.

Ilikuwa ndoa nzuri sana, kanisani palijaa furaha na palichangamka sana. Ninakumbuka mimi peke yangu ndiyo nilikuwa kama mtu ambaye nalazimisha furaha.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UKO HOME NIJE FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL

LOML | Love Of My Life FULL