LOML | Love Of My Life (03)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:03
Alicheka akisema β€œsi unaniona na shemeji yako?, sisi tupo tutumieni ili kuweka mambo sawa ndiyo maana ni walezi wenu. Hatupo hapa kusimama tu ina maana sana.”

Tukacheka na kukumbatiana. Baada ya hapa, watu walianza ingia kwa magari, na G sasa ananifuata na maringo yake ya kudeka β€œOoh baby lets go, twende Mine Man.”

Hapo tayari yupo mwilini, hata msimamizi ananitazama anacheka akisema β€œunaona mambo hayo, haya tangulieni kwa gari na mimi nimfuate babygirl wangu.”
Tulicheka tu.

Sasa nikiwa ndani ya gari, hapo mpenzi G na simu kila muda picha mpaka natamani kumwambia pumzika kidogo nipate hata kupumua nakasirika na la kufanya sina. Nikawa natazama tu dirishani, sielewi hata nifanye nini nipumzishe fuvu langu maana G ana hekaheka.

Si unajua wale wasichana kila kitu ni kuonyesha na wengine wajue anacho basi ndiyo G wangu. Ana maisha safi, msomi, pesa kwake sio shida ila kujisikia, na kujiona yeye ndiyo yeye hayo ndiyo maisha yake.

Basi akawa ananilazimisha ni tabasamu, nicheke ili mradi tu apate picha ambazo yeye anataka kwaajili ya matumizi yake. Nikawa sasa nimechoka. Wakati nikiwa natazama dirishani, upande wa pili kutoka pale tulipokuwa, nilimuona msichana mzuri sana, ninarudia tena, msichana mzuri sana sana sana.

Amevaa lubega, halafu mikononi ana fimbo sijui ni ya kazi gani ila alikuwa na fimbo. Na hiyo Lubega sio kwamba yupo wazi juu hapana inaonekana amevalia gauni kwa ndani sasa sijui sababu ya Lubega.

Jinsi alivyo tu nilijikuta natabasamu, na ilivyo ajabu nilikuwa nahisi kama ana tabasamu na mimi hata na mimi nikawa natabasamu kΔ±la nikimtazama. Huyu mwanamke ni mzuri sana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

KIBOKO YANGU FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL