LOML | Love Of My Life (06)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:06
Nakumbuka sana, nakumbuka usiku huu sasa tulienda fungate hotel kubwa sana hapo ni tunalala usiku huo na kesho ni safari kuelekea Zanzibar sehemu pekee ambayo mimi nilipendekeza badala ya Dubai, sikuona haja ya kwenda kote huko kutumia pesa wakati ninayo mambo mengi ingawa pia kwa Gabriella haikuwa rahisi kumshawishi.

Tulifika mpaka hotel, tulipofika sasa mke wangu, alinikumbatia na kusema β€œsasa ni mke halali wa Ricky, mpenzi wangu nakupenda sana, Wewe ni kila kitu nataka kukamilisha ulimwengu wangu. Wewe ukianguka tunaanguka wote, na ukiinuka tupo pamoja mpenzi wangu. Ricky mimi hapa mwenzako nakupenda si unajua babaaa eenh, na mtoto wetu akija atajivunia sana kuwa na baba na mama kama mimi. Nakupenda Ricky wangu.”

Nilimtazama na kutabasamu, halafu nilimwambia β€œWifey, nakupenda unajua hilo.”
Alitabasamu na kusema, β€œI know bedmate, nakupenda.”
Nilitabasamu, akauma mdomo wake wa chini na kisha aliniambia β€œbedmate leo nataka kuufanya huu usiku kuwa usiku wa kipekee sana, usiku wetu wa kwanza, hatujuani ndiyo tunakutana hapa. Nataka usiku huu unikumbuke kila mahali yaani. Ukiwa kazini, matembezini, barabarani, popote pale mpaka kwenye vikao unikumbuke mimi.”

Nilitabasamu na kisha nilimtazama nikisema β€œwaooo una maanisha?”
Alitabasamu na kusema β€œYes, kabisa bedmate naenda kuoga twende wote basi mpenzi.”
Nilimtazama na kusema β€œtangulia, nakuja.”
Alitabasamu.

Mke wangu huyu alipoingia bafuni, mimi nilibaki pale kitandani nimechoka. Sina hata hamu na mke wangu kiukweli kabisa. Hii fungate natamani iishie leo kesho mimi nirudi zangu kumtafuta yule msichana walau nimuone tena. Kuna kitu kimenikaa tu hapa, natamani kumuona mrembo yule tena na tena, natamani yeye ndiyo angekuwa hapa, ningekuwa na yeye hapa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

SIMULIZI YA INGIZA FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL