LOML | Love Of My Life (09)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:09
Mimi nikafumba macho yangu kama vile nimelala, mke wangu alipoona hivyo aliingia bafuni, mimi nikageuka upande mwingine ndani ya moyo wangu nasema β€œOoh Mungu wangu, ni nini hiki kimetokea, ni jambo gani hili?, kwanini umeruhusu ndoa kati yangu na Gabriella, ina maana nitateseka maisha yangu yote na ndoa hii nisiyoipenda kabisa. Mbona naona sasa ndiyo simpendi kabisa, sio mwanamke ninayemtaka mimi.”

Wakati huo Gabby alitoka bafuni, kisha alichukua simu yake na kwenda kukaa kwa kochi pale chumbani. Alikuwa ana amini mimi nimelala. Sasa anawasiliana na nani usiku wote huo na watu wanajua yeye yupo fungate.

Nitafanya nini?, inabidi niendelee kujifanya nimelala. Kukera inakera mwenzangu anatumia simu yake na mimi nipo tu hapo, tena kuna muda ana cheka. Ilikuwa kwa muda mrefu sana na baadaye alipanda kitandani. Sikufanya lolote mimi niliendelea kuwaza mambo yangu haga usingizi ulinichukua.

Asubuhi ilifika ambayo mchana wake tunatakiwa kusafiri. Kusema ukweli hii fungate naona kama isiwepo, nakereka tu na fungate, akili, moyo, mawazo yangu yote yapo kwa yule mwanamke. Hapo sasa mke wangu ameamka amevalia vizuri, ananiambia β€œbaby unaona hii nguo nilinunua bei gani unajua?”

Nilimtazama na kusema β€œunajua mke wangu una matumizi ya ajabu sana haya bei gani?”
Akacheka na kusema β€œushaanza hivyo mpenzi, pesa ikiwepo lazima itumike u know mimi kujibana siwezi na unajua.”

Nilitabasamu tu lakini ndani yangu nachukia. Mke wangu kununua nguo kwa laki 3 na kuendelea haoni shida na nguo ya ajabu, pochi ananunua bei za kutisha na ni vitu vya kawaida tu na hapo hataki ushauri.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

BIOLOGY TEACHER FULL