
LOML | Love Of My Life (10)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:10
Tulielekea kula, tulipofika kula mke wangu sasa anapiga picha kila kitu, mara nipige picha. Mimi tena ndiyo mpiga picha, chakula kinapigwa picha mpaka nachukia na ni muda wa kula. Alipomaliza alitabasamu na kusema βtule sasa Hubby.β
Nilishusha pumzi tu, alichukua uma wangu na kunilisha. Kisha aliendelea kula huku akiwa anazungumzia ndoa yetu namna imeenda viral, watu wanazungumzia, marafiki zake na zawadi.
Mimi nilikuwa nakula, namuwaza yule binti niliyemuona kanisani. Kisha nilikuwa nashindwa kabisa kujizuia kutabasamu. Nilijikuta natabasamu tena tabasamu pana kabisa. Mke wangu alinitazama na kuniita kwa Jina langu βRicky!!β
Mimi nikaendelea tabasamu, akaniita tena βRicky!!β
Nilimtazama na kusema βNaam!!β
Aliniuliza kwa kunishangaa βunatabasamu!!.β
Nikatabasamu tena na kumuuliza βkwani vibaya kutabasamu na mke wangu?β
Na yeye alitabasamu na kusema βkumbe nakufanya utabasamu, napenda hiyo mume wangu.β
Nilimtazama tu nikitabasamu kumbe mimi uzuri wa msichana yule ndiyo unafanya natabasamu na wala sio yeye. Moyo wa mtu kichaka. Tukiwa na hali hiyo mara simu ya mke wangu iliita. Aliitazama na kunitazama, nikamuuliza βkuna nini tena?β
Alishusha pumzi na kusema βni mama, sijui anataka kusema nini?β
Nilimtazama nikisema βpokea, labda wanakusalimia tu.β
Ndipo mke wangu alipokea simu, alipopokea tu nikaona uso wa mke wangu unapoteza furaha, nikamuuliza βkuna nini?β
Mke wangu aliendelea kusikiliza simu huku akinitazama kwa hofu, na kisha alikata simu na kusema β πππsa itakuajeπ€¦ββοΈπ€¦ββοΈπ€¦ββοΈ