
LOML | Love Of My Life (11)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:11
βDadie, ni mama, kazini mambo sio mazuri, tangu alfajiri baba anafuatulia na hakuna kitu anaweza kufanya sasa maana amechoka sana. Kuna kampuni tulikuwa tunafanya nayo kazi naona ina leta usumbufu na baba peke yake na meneja sidhani kama wataweza kama unavyojua mimi ndiyo nipo ofisini muda mwingi. Mume wangu, tunaweza kughairi hii safari kwa sasa then tutapanga upya walau sasa nimsaidie baba yangu?, tafadhali baby, please nakuomba.β
Nilitamani ajue namna nimefurahi, maana tu siku ya kwanza hii fungate ilikuwa imenichosha na kunipa mawazo sana kichwani. Nilikuwa sijaifurahia kabisa. Unaweza kuniona nina matatizo pengine au labda sina akili nzuri lakini niamini hivi ndiyo nilikuwa ninajisikia. Roho yangu juu ya mke wangu imeingia uzito sana. Nilikuwa naona kila kitu kibaya hapa.
Nilimshika mkono na kusema βpoleni sana mke wangu, mimi sina neno kabisa kwasababu hili ni jambo muhimu sana. Unahitaji msaada wowote ule kutoka kwangu?β
Gabriella alinitazama na kuniambia βnashukuru sana mpenzi wangu, najua nimekatisha wakati wetu mzuri sana. Nakuahidi nitalipia wakati huu Dadie. Sasa wacha twende nyumbani wewe ukapumzike na mizigo niache hapo halafu baada ya hapo niingie kazini.β
Nilimtazama na kusema βhakuna tatizo kabisa, kama unahitaji nikupeleke kazini pia ndiyo nirudi nyumbani ni sawa, hata kama unahitaji nikae hapo kazini nikusubiri pia ni sawa.β
Mke wangu alicheka kidogo, lakini tayari ninamfahamu suala la kazi uso wake tayari haukuwa na raha.
Mke wangu na mimi tulianza kurudi chumbani. Sasa hapa ndiyo nilianza kumuona namna anakuwa na kazi zake. Ni muda wote simu, akitoka kuzungumza na huyu anaongea na huyu. Nilikuwa namtazama tu, yeye akinitazama anatabasamu lakini haachi kuzungumza na simu na wakati mwingine maagizo yenyewe anarudia. Wakati mwingine tena anarudi kwa mama yake na kumuelezea namna anaweka mambo sawa basi vile akisifiwa mke wangu mimi ndiyo mimi huku kwangu mambo yanazidi ni simu simu na yeye.