
LOML | Love Of My Life (15)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:15
Na yeye aliniambia βusijali mwanangu, nitafanya hivyo.β
Nilitabasamu tu. Na huyu mama aliandalia kweli na kΔ±la mtu akaendelea na mambo yake.
Siku hii nilishinda hapa sebuleni, nilikuwa nimechoka sana nafanya tu kutazama hiki na kile na mazingira haya ni mapya kwangu basi nikichoka nainuka natoka natembea huku na kule hapa na pale walau tu kuona mazingira namna yalivyo na kuzoea.
Mpaka muda wa saa tatu mke wangu bado hakuwa amerudi lakini nilikuwa najua kinachoendelea hivyo haikunisumbua. Niliendelea na ziara yangu huku nikiwa ninajiambia ndani ya moyo wangu namna itakavyo kuwa atakapo rudi.
Nakumbuka mpaka saa 6 mimi nimechoka, Nimeingia chumbani nikaoga nikajitupa kitandani. Haukupita muda sana nikasikia geti linafunguliwa. Alikuwa ni mke wangu, nilisimama na kuchungulia dirishani, alikuwa ni yeye.
Nilijilaza uongo na ukweli kitandani walau akirudi nimpokee vizuri na uchovu wake. BaΕΔ± mke wangu anaingia ndani usiku lakini bado anaongea na simu. Alipofika nilianza kumtazama tu maana ni simu. Alipomaliza nilimwambia βKaribu mke wangu.β
Alinitazama na kusema βRicky wangu, nimechoka sana.β
Nilimtazama na kusema βpole sana mke wangu, massage?β
Alinitazama na kusema βmume wangu, Asante sana. β
Nikamuuliza tena βvipi umefanikiwa?β
Aliacha alichokuwa anafanya akanitazama na kusema βyaani mume wangu Hali ni tete sana. Baba peke yake alikuwa hawezi kabisa. Tumepoteza vingi najaribu kupambania walau tupate chochote. Hapa nilipo mume wangu, Nina maumivu ya moyo na mwili. Acha tu.β
Nilimtazama na kusema βpole sana mke wangu, unahitaji msaada wowote?β
Kabla hata hajajibu simu tena iliita, hapa sasa mimi ndiyo nilikuwa nachoka, hata ile hamu ya kumbembeleza iliniisha, nikajikuta najilaza huku na mimi nikichezea simu. Aliongea na simu yake, alipomaliza akaingia bafuni lakini hapo bado simu yake inaita mpaka nachukia sasa.