LOML | Love Of My Life (17)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:17
Nilitabasamu na kusema “naona nje pametulia, upepo safi kabisa.”
Akacheka na kusema “bwana harusi wangu karibu.”
Nikacheka tu.
Baada ya kukaa, na yeye alikaa akisema “karibu sana kaka, karibu.”

Mara mwanamke mzuri alitoka, alifika mpaka pale akaita “baby!!”
Willy alitabasamu na kusema “Mke wangu, huyu ni rafiki yangu sana. Anaitwa Rodricky, tunafanya pamoja biashara. Ricky huyu ndiyo shemeji yako.”
Nilitabasamu na kusema “Shemeji, nafurahi sana kukufahamu.”

Mwanamke huyu alivyo tu unatabasamu, ana zile tabia halisi za kike upole, ukarimu, woga, nidhamu.

Alikuwa anatabasamu akisema “karibu sana shemeji yangu, jisikie huru kabisa.”
Nilitabasamu, na kisha alisema “baby samahani, nakuomba mara moja.”

Willy na mke wake wakashikana mikono na kusogea pembeni mimi nawatazama tu. Ukiwaona tu unajua kabisa hapa kuna upendo. Baada ya muda kidogo Willy akarudi akisema “Ricky!!, niambie kaka.”

Nilitabasamu tu, mke wake alirudi na vinywaji, kwa heshima aliandaa na kisha alitukaribisha kwa tabasamu na kuondoka zake.

Mimi nilimtazama Willy na kusema “hongera, una mke mzuri sana. Mpole, msheshi na mwenye heshima sana.”
Willy alitabasamu na kusema “namshukuru sana kwa hilo kusema kweli, namshukuru.”
Nilitabasamu tu.

Tuliendelea kunywa pale rafiki yangu aliniuliza “Ricky shida nini kaka?”
Nilimtazama na kusema “nimetafakari sana maneno yako, ninaona nijipe nafasi kwake. Lakini unajua nini kaka, sina amani kabisa, kuna muda naona bado sikutakiwa kuingia kwenye hii ndoa, naona kabisa.”

Willy alitabasamu na kusema “sijui sana kuhusu mwanamke wako, sijui sana kuhusu maisha yenu, ila kitu pekee najua ni kuwa mnapendana ndiyo maana mmefikia hatua hii. Yape mahusiano yako nafasi, mpende, muoneshe una mjali, mthamini na mengine yatakuja tu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata