LOML | Love Of My Life (19)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:19
Willy meno yote nje, halafu alisema akimtazama β€œNashukuru sana mke wangu.”
Nilitabasamu, ile raha inanizidi tu moyoni, shemeji alinitazama, halafu mpaka anadidimia fulani hivi β€œShemeji karibu ndani tafadhali, chakula kipo tayari.”

Halooo, mimi kwanza mwanamke kuniongelesha hivi kwa heshima ya kiwango hiki haijawahi kuwa. Basi nilikuwa nashangaa tu. Shemeji aliingia ndani kwake, mimi nilimtazama Willy na kumuuliza β€œBro!!, huyu mwanamke umempata kijiji gani?”

Willy alicheka na kusema β€œkijiji wapi, wanawake wazuri mjini hapa wapo wengi sema wanaume mnajua mnachotaka mimi nilikuwa na jicho, jicho la mbali sana.”

Nilijikuta natabasamu na kusema β€œsijawahi kupata heshima kama hii, hata mama yangu kwa baba naona wanaishi tu wenyewe.”
Tukacheka huku akisema β€œwazee tena wanajuanaga hao.”

Tulicheka, ila kusema ukweli kutoka ndani ya moyo wangu. Kuna jambo kubwa ambalo lilikuwa limenivutia hapa. Upendo, upendo sio mke na mume tu na mtoto wao. Mezani mpaka dada wa kazi ameketi hapa.

Na kwa upendo tunakula, Willy na mke wake wanalishana basi mimi natabasamu tu. Kusema ukweli mke wa Willy anaishi vizuri sana na mume wake sijui mengine ila kwa haya machache nashukuru Mungu nimejifunza kitu.

Chakula kilikuwa kizuri sana na nilifurahia. Nilimshukuru Shemeji kwa chakula na kusifia kwa heshima kwamba chakula kizuri sana na nimefurahia. Ulikuwa wakati mzuri sana. Muda wote nipo hapa natamani Gabriella angekuwepo hapa. Kwasababu yeye na maisha ya namna hii ni vitu viwili tofauti kabisa. Nilifurahia sana. Kwakuwa nilikuwa tu sina la kufanya nilishinda hapa. Lakini pamoja na kushinda hapa mke wangu hakuwa amenitafuta.Nilikuwa natamani kuongea naye, nataka sasa ule ukaribu sana na mke wangu ili tutengeneze bond lakini haikuwa hivyo.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

KIBOKO YANGU FULL