
LOML | Love Of My Life (20)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:20
Kuna kitu kilinijia kichwani, kumbe maisha ya mapenzi au mahusiano ni mazuri sana kabla ya ndoa kwasababu mkiwa mbali mnakumbukana. Hii kuamka pamoja kila siku ni ngumu sana. Kuzoeana kule kuna weza kuwa na faida hasi au faida chanya.
Niliagana na Willy na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Mida ya saa tatu ndiyo nilirudi nyumbani. Nilikutana na huyu mama yetu hapa. Nilimsalimia kwa upendo sana. Na nikamuuliza βvipi mke wangu amerudi?β
Aliniambia kwa upole βhapana bado hajarudi. β
Mimi simjui sana huyu mama ila mke wangu ana mfahamu maana ameishi naye kabla. Hivyo niliingia tu ndani hata kula sikula maana nahitaji mke wangu sana kuliko kingine.
Nilioga, na nilipo maliza nilipanda kitandani na kumpigia mke wangu. Mke wangu alipokea simu. Niliita βmke wangu!!β
Nikawa simsikii yaani sehemu alipo pana kelele sana. Nikamuuliza βmke wangu upo wapi pana kelele sana?β
Simu ilikata, nilibaki hata sielewi. Nikapiga tena haikupokelewa na mwisho niliamua kulala tu maana sikuwa na namna kabisa.
Nililala, nililala na uchovu wangu, sijui hata mke wangu alirudi saa ngapi ila saa 11 hivi mke wangu alikuwa ananipapasa. Nilijivuta karibu yake na kusema kwa sauti ya usingizi βWifey, umerudi saa ngapi?, nimekusubiri sana.β
Na yeye kwa kudeka aliniambia βbaby, nilichelewa kidogo. Lakini habari njema ni kuwa nimemalizana na ile suala lakini inaumiza sana tumepoteza sana mume wangu.β
Nilifikicha macho na kusema βpole sana baby, ndiyo biashara.β
Mke wangu alisema βnakuhitaji hubby, i need you please.β
Mimi tena hapa ndiyo nimetaka mke wangu ajisikie yupo na mimi. Nataka kudumisha ndoa yangu vizuri kabisa na siku ya jana imepita leo lazima nifurahie na mke wangu afurahie. Sikuwa mbishi nilimsogelea mke wangu.
Mke wangu alinisogelea kwa mahaba, unajua nashindwa kukuambia kwa uzuri ukanielewa. Nilisema huku mwanzo kuwa mke wangu anapenda mapenzi na hachoki. Sasa endelea kunifuatilia vizuri, hatua kwa hatua utanielewa tu.