
LOML | Love Of My Life (24)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:24
Nasoma baadhi ya waandishi lakini hali ilivyokuwa na ninacho soma naona ni mambo tofauti sana. Sioni ule uchungu au yale maumivu mimi mke wangu alikuwa sawa kabisa mpaka niliposema.
Nilisoma mengi kuhusu bikra, basi maumivu kutofautiana na hata wengine damu kutoka kwa wingi, wengine kidogo kwa namna tofauti tofauti. Unajua nasoma kuridhisha nafsi yangu kuwa nilifanya kosa.
Tangu ile siku mpaka inafika jumapili, mke wangu hakutoka kitandani, na wala hakutaka nimguse kabisa. Nilielewa, niliamini pengine ana hasira na mimi hivyo nimefanya kosa niwe mpole. Nakumbuka jumapili hii nilimwambia βmke wangu amka twende hata kanisani.β
Alinitazama na kusema βkanisani?, hapana Mume wangu wewe nenda tu katubu mwenyewe mimi hapana.β
Kauli hii ya mke wangu ilikuwa inanifanya kama vile ndiyo naingia motoni moja kwa moja. Nilimtazama na kutoka zangu, nilipofika ndani ya gari nililia sana, mwanaume nililia na uchungu natamani hata nimwambie baba yangu pengine labda atakuwa na la kusema lakini naanzaje kusema hili.
Nilijikaza na kuondoa gari huku nalia. Kanisa ambalo tulifungia ndoa lilikuwa mbali kiasi chake. Niliacha la karibu niliendesha gari mpaka lile kanisa. Nilichelewa kidogo, nikaingia kanisani.
Nilisali na muda wa kutoka nilibaki nimekaa mwisho machozi yananitoka. Namwambia Mungu wangu βnakuomba sana Mungu, jambo hili lisichukue akili yangu. Sikufanya makusudi. Nakuomba Mungu, nisaidie, niondoke kwa kifungo hiki. Naona naelemewa kwasababu sijawahi kuwaza kukuudhi hata mara moja.β
Nilitokwa na machozi sana. Taratibu nilianza kutoka nikitazama huku na kule pengine nitapata bahati nyingine tena ya kukutana na mrembo yule walau hata kwa mbali au nimsalimie. Niliangaza huku na kule lakini sikumuona. Na ukiniuliza una mtafuta wa nini wakati umeamua kumpenda mke wako mpaka leo sina jibu. Nilikuwa najikuta tu katikati ya hali hii.
Niliingia ndani ya gari yangu na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Kiukweli kabisa hali yangu haikuwa nzuri, ninamuhitaji mke wangu, mimi mwanaume unajua, mke wangu mzuri, anavutia lakini bado amenikasirikia.