
LOML | Love Of My Life (28)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:28
Nilikuwa navaa huku hata mikono ina tetemeka, mke wangu alinifuata na kupiga magoti mbele yangu analia machozi kama yote. Vile anajua kusema mume wangu sasa. Hapa ni βMume wangu, nakuomba sana Mume wangu, Mume wangu usiniache nisikilize mimi nakuomba Dadie, dadie please eenh, unajua nakupenda, Dadie wewe ndiyo kila kitu nataka. Please Baby wangu, please listen to me, babe tafadhali.β
Nilimtazama na kumwambia βwewe ni kitu kibaya kwangu, wewe ni hatari sana Gabriella, sina hata kitu cha kukulinganisha na wewe. Una roho mbaya na tabia mbaya sana. Siwezi kukusamehe kwenye hili, siwezi kukusamehe kwenye jambo hili kamwe kabisa sitaweza. Sijui hata nikufananishe na nini?.
Kifupi kuhusus hili, Gabriella kwenye hili sidhani kama utaniambia chochote na sioni kabisa uelekeo wa ndoa na mwanamke mshenzi kama wewe, ndoa yetu hata mwezi haijafika mwanamke mwenyewe ni mshenzi namna hii. Wewe si unaweza hata kuniua wewe na ukakataa. Kila nikikutazama natamani nikupasue kichwa chako.β
Akawa ananisogelea, ananishika miguu, analia akisema huku anadeka βDadie please!!, nakuomba mpenzi wangu, baby wangu please mume wangu please!!. β
Natamani kama ungesikia hii sauti yake, anadeka Gabby huyu, anadeka mpaka unaweza kukaa ucheke tu, anadeka sana. Maneno anavyotamka.
Nilimsukuma na kusema kwa hasira hapo nishamaliza na kuvaa βtoka hapa mbuni wewe, Dadie please!!, Dadie pleaseee, sikiliza mamie, usinuguse, usiniguseee mimi.β
Nilimsukuma akaa chini kabisa hapo yeye kajifunika tu shuka, mimi nilimtazama na kisha kwa hasira nilitoka.
Humu ndani kuna mimi na mke wangu na msaidizi wa kazi. Lakini namna nilivyo toka sina hakika kama niliondoka vizuri kwa maana nilikuwa na hasira sana. Nahisi kabisa pengine hata nimemkosea mtu heshima.