LOML | Love Of My Life (29)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:29
Ni moja kwa moja ndani ya gari, nilipofika hapo niliwasha gari yangu, mlinzi alifungua na safari ilianza. Niliendesha gari kwa hasira, baadaye hata ndani ya gari najiambia β€œtulia Ricky, utapata matatizo hasara kwako wewe mwenyewe. Tulia nakuomba.”

Nilisimamisha gari haraka, nilianza kupiga ule usukani nikisema β€œni yeye mwenyewe, makusudi, amezoea ndiyo maana haumiii, ndiyo maana halalamiki, amezoea.”

Nililia pale kwenye usukani huku nakumbuka zile kelele. Nikisema kelele sio poa, kelele ni kelele nyingi sana tena za raha. Mke wangu ana furahia sana mpaka unaweza kuchanganyikiwa ukaendelea na kutenda ujinga huo.

Roho yangu kila ikikumbuka hivi naumia, sasa ndiyo maana nilikuambia kidogo kidogo utanielewa. Hii ni simulizi yangu ambayo ina matukio mengi makubwa makubwa. Sasa nawaza ndiyo sababu sijawahi kuhisi mke wangu ametosheka kuanzia uhusiano.

Mnaweza mfanye mapenzi mpaka wewe ukawa hoi mwenzio wala kumbe kuna mahali yeye anafurahia. Kitu pekee kinaniuma roho yangu, kitu pekee kinanitesa nafsi yangu ni kuwa mimi kama mwanaume wake, mume wake, hata siku moja, hata mara moja sijawahi kumfanya mke wangu kinyume na maumbile yake.

Na kwa namna anapenda ina maana kuna mwanaume ana mfikisha mke wangu.Kuna mwanaume ndiye ana mburudisha. Ina maana mke wangu ananisaliti.

Nililia machozi nikisema β€œhapana, Gabriella hawezi kufanya hivyo, kwanini anisaliti, anatafuta nini kunisaliti mimi. Ricky acha kuwaza ujinga.”


Niliwasha tena gari, hata nilikuwa sijui naenda wapi kusema kweli, niliendesha gari mpaka nyumbani, kwa baba yangu na mama yangu. Nimefika.

Sasa najiuliza β€œnaenda kumwambia nini mama?, baba nawezaje kunwambia kuhusu hili?. Sikupaswa kuwa hapa, inanibidi niondoke tu.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

JOGGING MASTER FULL

KIBOKO YANGU FULL