
LOML | Love Of My Life (30)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:30
Vile narudi ndani ya gari ili niondoke, nasikia sauti ya baba yangu ikisema βkaribu sana kijana wangu. Nimefurahi sana kukuona.β
Nilitabasamu na kusema βbaba yangu.β
Hapo nilikuwa nazuga tu ila ukweli ni kuwa nilikuwa nataka kuondoka.
Baba yangu alinifuata na kunikumbatia, ananipenda sana baba yangu. Nilimkumbatia pia. Baba alinitazama na kuniuliza βmkwe wangu yupo wapi, mnatakiwa kuwa wote.β
Nilitabasamu huku moyoni naumia.Laiti wangejua huyo mkwe ni mjinga na mpumbavu ndiyo amenifanya kijana wao niwe hapa bila kupenda. Nilijifanya nachekacheka nikisema βnilikuwa napita mitaa hii nikaona niwasalimie. Mama yuko wapi?β
Baba alinitania akiwa ameshika mkono wangu βunatakiwa kutembea na mke wako bwana wewe bado kijana ringa na mkeo.β
Nilitabasamu tu huku tunaingia ndani, lakini tulipofika mlangoni baba yangu aliniuliza βupo sawa kweli mwanangu?β
Nilimuuliza baba yangu βkwanini baba?β
Alinitazama na kisha mikono yangu halafu na mimi nikajitazama. Baba yangu alisema βunatokwa na jasho, macho yako, uso wako, sikuoni kuwa sawa kama kuna tatizo niambie, mimi ni baba yako.β
Nilitabasamu tu na kisha nilisema βnimechoka sana baba, kuna muda ni kama homa inani nyemelea hivi mwanao. Ila nitakuwa sawa.β
Baba alisema kwa upole βpole sana mwanangu, uchovu na vipi kazi umeanza?β
Tukawa tunaendelea kuingia ndani huku namwambia baba yangu namna ambavyo ndiyo najiandaa wiki linalofuata nianze kazi.