LOML | Love Of My Life (32)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:32
Nilikaa kitandani na kujiinamia nikiwaza. Akili yangu inawaza mambo mengi haswa natamani kujua zaidi kuhusu mke wangu. Hivyo ndiyo akili yangu inaniambia, akili yangu inataka kumjua mwanamke ambaye naishi naye ili nijue hizi hisia za kuwa mzito na ndoa hii ni sawa au ni hisia tu.

Na kama ni sawa Mungu kwanini ameniacha niingie kwa ndoa hii na mwanamke wa namna hii lakini, ni mwanamke gani huyu?, nashindwa hata namna ya kulalamika kwa Mungu wangu kwasababu mimi ni mtu naelewa kabisa Mungu alivyo. Nisikie nakuambia hapa, hakuna kitu kinatokea kwenye maisha yako bahati mbaya. Hata kama ni kidogo namna gani, chunguza kilipotokea ikawaje?.

Hakuna bahati mbaya kwenye maisha kila kitu kinatokea kwasababu kitu fulani kitokee na kiwe funzo kwako au wengine, kikuvushe, kikufikishe mahali, haijalishi ni kizuri au ni kibaya lakini kimetokea hapo kwasababu tena sababu kubwa na maalumu kabisa.

Tena wakati mwingine unalia kabisa unaona Mungu hakujibu. Kumbe hilo unalo ona limebaki vilevile, au hali imekuwa mbaya zaidi, au kinyume cha ulivyo omba ndiyo jibu la maswaki yako. Mungu anajibu kwa namna mbalimbali tena namna za kipekee kabisa.

Unataka hayo ndiyo majibu sahihi kwako hutaki hayo ni majibu sahihi kwako. Mungu yeye anajua sababu ya kwanini majibu hayo.

Yapokeee na ujue unapita vipi hapo kwa hekima. Mungu anakupa unacho stahili, anakupa kinachokufaa na kumpendeza, sio kile unataka wewe. Kuna namna za kukifikia hicho unataka taratibu taratibu nenda na Mungu.

Nikiwa pale kitandani kumbe baba yangu ameingia maskini hata sijamuona nimejiinamia tu nawaza mambo kichwani napanga na kupangua na kwa bahati mbaya jambo nawaza siwezi kumwambia mtu. Ninawezaje kumwambia mtu mke wangu anapenda mapenzi ya kutisha namna hii. Ninawezaje kumwambia baba yangu kuhusu jambo hili, sio baba yangu tu hata mtu yeyote yule. Ni ngumu sana, sio rahisi kabisa. Inaumiza nafsi.

Nilishangaa naguswa tu begani, nikainua uso wangu. Vile nimeinua uso wangu sasa umejaa machozi. Baba yangu alinikumbatia na kunibembeleza wanaume vile tunabembelezana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata