LOML | Love Of My Life (34)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:34
Kitu pekee unatakiwa kufanya kijana wangu ni kuipambania ndoa yako, kuhakikisha kıla kiti kinakuwa. Sio rahisi mwanangu tena wakati mwingine ni ngumu haswa. Lakini usikubali kushindwa wewe ni mwanaume na ndoa yako hata mwezi bado tafadhali. Simama imara.”

Nilimtazama baba na kujikuta namuuliza “umewahi kukaa siku ukajutia kumuoa mama yangu, au kuhisi humpendi kabisa?”

Baba alinitazama kwa muda, nikaona macho yake yakibadilika. Halafu baba yangu alitazama chini. Nikaona anainua mikono yake na kujifuta machozi. Halafu nikaita “baba!!”

Baba aliinua uso wake akitabasamu japo naona hayupo na tabasamu La awali na kusema “kuna mtu kijana wangu huna La kufanya kabisa una acha tu maisha yafanye vile yanataka. Ndiyo maisha. Inatokea Mara nyingi lakini sio sababu ya kuacha ndoa yako. Wakati mwingine suluhu ni kutulia tu.”

Nilimshangaa baba yangu, wakati huo mlango ulikuwa unafunguliwa, alikuwa mama akitabasamu na kusema “baba na mwana, mna kikao gani cha Siri namna hiyo?”
Tulijifanya kucheka tu, halafu mama aliniuliza “Upo sawa lakini?”

Nilitabasamu na kusema “kabisa mama, hata hivyo nataka niwahi nyumbani.”
Mama alitabasamu na kusema “kabisa maana binti yangu alipiga anaonekana na wasiwasi sana. Kıla kitu kipo sawa lakini.”

Nilimtazama mama na Kisha baba nikainuka pale nikisema “kila kitu ni sawa kabisa. Baba uwe na usiku mwema, mama yangu Nakupenda sana. Mimi niwaache sasa.”

Sikusubiri hata jibu, nikawa natoka huku nasikia mama anaita “Rodricky, wewe Rodricky, Ricky mwanangu.”
Baba ana mwambia “mke wangu, Muache mtoto. Muache aende.”

Sijui waliendelea kuzungumza nini, mimi niliingia kwa garı yangu, niliwasha garı na kuanza safari ya kutoka pale nyumbani.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata