LOML | Love Of My Life (35)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:35
Nikiwa nishatoa gari nilichukua simu yangu, lengo lilikuwa nimtafute Willy, pengine Labda nitaweza kuongea naye. Nilichukua simu. Nilikuta mke wangu amenipigia sana. Missed call nyingi sana. Nilitazama na kushika simu yangu kwa nguvu zote. Nilikuwa natamani kama yeye ndiyo awe ile simu lakini inawezekana vipi.

Nilitazama machozi yanatoka. Kıla nikikumbuka vituko vya nje wangu ndiyo nazidi kuumia. Aliniandikia ujumbe akisema “Dadie tafadhali, nakuomba sana, usinifanyie hivyo. Wewe ndiyo kila kitu nahitaji, wewe ndiyo sababu nipo hapa leo.

Hujui tu ni namna gani umenisaidia, uwepo wako umeongeza mengi sana kwenye maisha yangu. Wewe ni nuru yangu, mwanga wangu Ricky. Nakuomba tuzungumze, nakuomba mpenzi, mume wangu nisikilize nakuomba sana. Haki ya Mungu Nakupenda sana.”

Sikutaka hata kuhangaika naye, nilimpigia simu Willy. Alipokea na aliniita “kaka niambie.”
Nilikosa cha kusema hata akasema “hello, kaka unanisikia?”
Nilijikaza na kumuuliza “upo wapi bro!!”
Willy aliniambia alipo akisema “sina muda mrefu hapa, kuna vitu wife aliniagiza namchukulia Kisha narudi nyumbani.”
Nilivuta pumzi na kusema “nisubiri.”
Willy aliniuliza “Kwema kaka?”
Mimi nilikata simu yangu, nilipokata tu simu ya mama yangu iliingia. Nilipokea, mama yangu aliniambia “mwanangu mwenzio yupo hapa wewe upo wapi tena?”
Nilishangaa, Ina maana mke wangu amenifuata mpaka nyumbani. Nilimwambia mama “mwambie arudi nyumbani mimi narudi sio muda.”
Mama aliniuliza “kuna usalama lakini?”
Nilimwambia mama yangu “kila kitu kipo sawa mama.”
Mama alisema kwa upole “sawa mwanangu, ninawaombea sana, mpendane na kusikilizana. Ndoa yenu idumu milele.”
Nilivuta pumzi ile kujibu amina mpaka machozi yaani “amina mama.” Na machozi juu.

Nilikuwa nashindwa kuelewa ni mwanamke wa aina Gani nimeoa. Mwingine kwake ni kawaida Labda pengine kwasababu siku hizi mambo haramu yana kuwa mazuri na kupigiwa kampeni.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata