LOML | Love Of My Life (36)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:36
Upande wangu mimi hili limenishtua. Ni Kama kengele ya hatari imelia kichwani kwangu. Kengele ambayo Ina amsha mambo mengi. Najua unataka kujua nawaza nini?.

Hapa nilipo nawaza Nani anamfanyia hivyo mke wangu, nawaza ameanza lini, ana mtu mwingine nje ni nani huyo, zile kelele anazopiga, kelele za raha na kufurahia tendo haramu anafanya na nani. Ina maana mimi kwake ni kama nacheza tu simfikishi popote na kujituma kote ninavyo jituma, mwanamke yeye ndiyo anataka vile sio mimi hii kwangu ni hatari.

Naendesha garΔ± kwenda kwa Willy Ila kichwa kinawaka moto. Muda huu hata nilimkumbuka Willy na familia yake, namna wanaishi, namna alivyo na mke mstaarabu hata anamuagiza vitu haoni taabu kupitia.

Nilifika nje ya ile SΓΌpermarket aliyokuwepo Willy, na nilimpa taarifa. Nimefika halafu sasa najiuliza β€œHivi nimekuja kufanya nini, nitamwambia nini Willy kuhusu hili?. Ni aibu, linatisha siwezi kusema, siwezi kumwambia kitu kama hiki. Mungu wangu!!, Mungu wangu!!, Mungu wangu, nimeoa nini mimi.”

Nikiwa katika Hali hiyo ya kuwaza hili na lile Willy alitoka. Nilimuonesha ishara nilipo na alikuja mpaka nilipokuwa. Nilimfungulia mlango wa gari akaingia. Aliponiona tu alipoa, kwa kunitazama aliniita β€œRicky kaka, salama kweli?”

Nilishusha pumzi na kumtazama, Kisha nilisema β€œsalama kaka, nisamehe nimekusumbua nilitaka kukuona tu.”
Alinitazama na aliniambia β€œnipo hapa, niambie shida ni nini?”

Nilishindwa kumtazama usoni, hivi nawezaje kumsema mke wangu kwa rafiki yangu kuwa anafanya mapenzi kinyume na maumbile ndiyo ana furahi.

Kusema ukweli sijui kuna wanaume wanakutana na hili langu au mimi ndiyo linanishangaza Kiukweli linanipa taabu sana. Naona ni kubwa sana, linanitesa sana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata