
LOML | Love Of My Life (38)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:38
Akaniambia kWa upole βShem, sitaki kuwaingilia kabisa, lakini nakuomba sana Shem. Chochote mnachopitia tafadhali kaeni chini muyamalize. Ndugu yangu analia sana, ananiambia amekukosea tafadhali msamehe ingawa sijui nini kimetokea. Tunawapenda na tunatamani ndoa yenu idumu.β
Nilimuuliza βShem, amekuambia alichokifanya?β
Shem aliniambia βhapana hajaniambia analia tu muda wote, naomba Shem zungumzeni mmalize hili nakuomba.β
Nilimwambia βGiana shemeji yangu, ongea na ndugu yako. Mwambie asinione mimi mpumbavu. Mimi Nina akili zangu timamu na nikirudi nyumbani awe na majibu kamili ya maswali yangu vinginevyo.β
Giana ni rafiki yake Gabriella wa muda sana . Lakini tofauti Yao ni kuwa huyu Giana ni amekaa kiheshima sana tofauti na Gabriella, huyu amekaa kiheshima na hata alivyo ana heshima sana.
Ni rafiki mzuri sasa sijui na yeye ana danganywa kama mimi, na yeye hamjui vizuri anaye muita rafiki na pengine ndiyo maana hajamuambia alichofanya.
Nilipokata simu Giana alinitumia ujumbe βnisamehe sana shemeji yangu kWa usumbufu. Nina amini utamsamehe rafiki yangu kwaajili ya Mungu. Tafadhali sana Shem. Haipendezi kugombana mapema hivi. Tunawaombea mpate amani na mfurahie. Nawapenda sana.β
Nilisoma tu huku moyoni nikisema βmngejua msingekuwa mnanifanyia hivi kabisa.β
Si kumjibu Giana, lakini maneno yake na Willy ni Kama yalikuwa yanataka amani tu. Lakini kumuwaza mke wangu peke yake ilikuwa inaniua.
Siku rudi nyumbani moja kwa moja. Nilifika mahali niliagiza Kinywaji pale nikawa nakunywa huku nawaza nyumbani. Kuna vitu ukiwaza acha tu. Mimi naona kabisa ndiyo nimekuwa mtoto wa shetani. Naona mwanamke huyu amenipeleka jehanamu kWa kunifanyisha kitu sijawahi tamani hata ndotoni. Roho inaniuma sana.