
LOML | Love Of My Life (39)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:39
Mke wangu alikuwa anapiga sana simu, simu ilikuwa inaita sana lakini sikuwa najali. Sikuwa napokea. Meseji ndiyo usiseme. Mke wangu analalamika “baby please, nakuomba mume wangu nimeenda mpaka nyumbani sijakukuta. Upo wapi mume wangu. Tafadhali nakuomba.”
Text na emoji za kulia Kama zote. Mimi ninatazama tu simu na Nakumbuka mida ya saa tano hivi ndiyo nilianza safari ya kurudi nyumbani.
Nilifika nyumbani, nilichelewa kusema kweli na kuchelewa nyumbani sio kitu mimi Napenda Ila imekua na sina namna. Nilipofika nikaingia ndani. Nilipoingia tu nilimkuta Giana na rafiki yake akiwa Analia. Giana aliponiona alinitazama kwa upole na kusema “Shem Karibu.”
Niliitikia kwa ustaarabu kabisa “Asante shem, upo hapa.”
Giana aliniambia “sikuwa na namna niliona nije tu Ila kwakuwa umefika Naomba niwaache please shem zungumzeni.”
Mke wangu alisimama na kusema kwa upole “karibu mume wangu.”
Nilimtazama tu, Kisha nilimwambia Giana “nikupeleke ni usiku sana.”
Giana alinitazama na kusema “Usijali Shem, mume wangu atanifuata tu hakuna shida. Hayupo mbali na hapa ndiye alinileta.”
Nilimtazama na kusema “pole kWa usumbufu, karibu sana utamsalimia sana bro.”
Giana alisema kwa upole akitoka “Asante sana shem, Rafiki yangu uwe na usiku mwema. Tafadhali zungumza vizuri na mumeo.”
Sikujibu kitu badala yake mimi nilianza safari ya kuelekea chumbani. Haraka mke wangu alipiga magoti na kushika miguu yangu akilia kwa maumivu akisema “mume wangu tafadhali nisamehe, nakuomba mume wangu.”

