LOML | Love Of My Life (44)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:44
Anajua sana kujitetea, lakini ukweli kabisa kabisa hili jambo lilikuwa linaniuma kuliko kawaida. Lakini hadithi yake sijui ni ya kweli au ni uongo nilijisikia vibaya. Kuna wanaume tu wapo kutumia vibaya wanawake vile wanajua na wanaita upendo. Watu wanakuwa addicted na vitu vibaya na hawawezi kujinasua.

Nilimtazama kwa upole nilisema β€œacha kulia, inatosha.”

Sikutaka hata jibu, niliingia bafuni, huku sasa ndiyo na mimi niliweza kupunguza maumivu yangu kwa kulia. Nilikuwa nimefungulia maji naoga huku machozi.

Ndani yangu nilikuwa natamani kumjua zaidi huyu mwanamke. Kuna wakati mwanamke au mwanaume tabia zake ndiyo zinalazimisha uanze mfukunyua. Mimi nilimpenda mwanamke huyu bila kutaka kujua chochote kumuhusu yeye.

Lakini tabia zake ni zinaonesha simfahamu kabisa mwanamke huyu, simfahamu hata kidogo. Kitu pekee najua kuhusu yeye ni kazi na familia maisha binafsi sijui kitu chochote kile. Nilitumia muda sana bafuni. Niliwaza Mengi haswa ni kumfahamu huyu mwanamke Gabriella.

Nilipotoka bafuni sasa, nilipitiliza kitandani bila hata kuzungumza kitu. Niliona Mke wangu amesimama tu hanigusi hata ananitazama tu. Mimi sikujali nikajilaza vizuri zaidi. Nikamuona mke wangu na yeye anaenda zake bafuni. Alikaa sana huko pia. Aliporudi na yeye alipanda kitandani.

Akawa anataka kunikumbatia lakini nilimtoa mikono yake sitaki hata aniguse. Kusema ukweli hili lililotokea limenikata sana. Kuna hali najisikia au nikimuona napata hasΔ±ra kabisa. Alikuwa mpole tu, alitazama upande mwingine na mimi nilitazama upande mwingine sikutaka hata kusumbuka kabisa. Nililala.

Usingizi ulinichukua kabisa ni wazi hasira na kuchoka vilinifanya niupate usingizi kwa urahisi sana. Nililala usingizi mzito. Nikiwa nimelala sasa, nilikuwa naota ndoto, ndoto nzuri sana. Nzuri kwasababu nilikuwa na furaha sana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SIMULIZI YA INGIZA FULL

LOML | Love Of My Life FULL

KIAPO CHA MASIKINI FULL