
LOML | Love Of My Life (45)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:45
Nilikuwa nipo na msichana Yule niliyemuona siku ya ndoa yangu kanisani.Tulikuwa tunacheka sana, tunacheza sisi wawili kwenye mvua huku tukitaniana na michezo ya hapa na pale.
Nikiwa na furaha namna hiyo nilimuona mke wangu akija na hasΔ±ra. Alipofika kwa Yule msichana alisema βunafikiri ni rahisi hivyo, unafikiri nitakuacha tu umchukue Mume wangu kutoka kwangu.
Huyu ni mume wangu, mume wa maisha yangu kamwe huwezi kumchukua. Ni Bora nife mimi, ufe wewe au yeye lakini hakuna wewe kuwa na mwanaume wangu, Hilo futa, futa kabisa kwenye akili yangu.β
Mimi nilisogea karibu yake na kusema βmke wangu tafadhali acha, Muache msichana huyu.β
Mke wangu alipiga kelele akisema βNi wangu, Rodrick ni wanguuuuuuuuuuu.β
Nilishtuka na kushika kifua changu, lakini nilipo mtazama yeye alikuwa amelala tu, alikuwa amelala ametulia kabisa.
Nilishusha tena pumzi nikisema βIna maana ananipenda kweli huyu mwanamke?. Sasa Kama ananipenda ni kwanini imani yangu kwake inanipungua kila siku, kila siku inanipungua hii imani.β
Nilimtazama tena, nilitamani kushika simu ya mke wangu. Lakini sikuwahi kushika simu ya mke wangu kamwe kwenye maisha yangu Kwahiyo sijui kitu chochote.
Nilimtazama na Kisha nilisema βnitaanza kukufuatilia kuanzia sasa mke wangu, kwasasa sitafanya lolote na wewe, chochote kile mpaka pale nitakapo ona mambo yanakaa vizuri na moyo wangu una amani ndiyo nitajua nini nifanye.β
Niliinuka na kuingia zangu chooni lakini Baada ya muda nilitoka na kurudi kitandani huku natafakari kuhusu ile ndoto. Huku ndani yangu najiuliza kuhusu Yule msichana wa kanisani. Ni nani na mbona sijawahi kumuona tena tangu nifunge ndoa ni mwezi sasa unaisha lakini sijawahi kumuona tena hata pale kanisani.