LOML | Love Of My Life (46)

Β 

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:46
Nilipokuwa nawaza hayo usingizi ulinichukua tena. Safari hii niliamshwa kwa upole na sauti ya Gabriella mke wangu. Aliniita kWa upole β€œMume wangu!!, Mume wangu!!, amka kipenzi chai ipo tayari.”

Nilipo fungua macho yangu nilimuona akiwa amependeza mwenyewe unajua ni mrembo sana. Nilimsalimia kwa upole β€œGoodmorning!!”

Alitabasamu na kusema kwa upole β€œMorning hubby, umeamkaje Dadie?”
Nilimtazama na kushusha pumzi nikisema β€œnipo salama kabisa.”

Başı niliinuka na Kisha kutazama muda, ilikuwa ni saa nne asubuhi. Nilisema kWa sauti ndogo β€œnimechelewa, tangulia nakuja.”

Alinitazama na Kisha aliniambia tena β€œMume wangu kipenzi, tafadhali nisamehe sana. Ninajitahidi kuwa mke mzuri kwako. Nakuomba nisamehe Nipe nafasi nyingine.”

Nilimtazama pasΔ± kusema kitu na yeye akawa anatoka na mimi nilishusha pumzi na kuingia bafuni. Nilijiweka safi haraka haraka na nilitoka kwaajili ya kupata chai. Na wakati nimefika mezani Yule alikuwa anamalizia kuweka meza sawa na kuondoka zake. Niliita β€œmama Babuu!!”

Alinitazama na kusema β€œNaam boss!!”
Nilitabasamu na kusema β€œkwanini usikae hapa tule pamoja na badala ya kila siku kula ukiwa jikoni.”

Mke wangu alinitazama na kusema akitabasamu β€œmume wangu Muache tafadhali, alishakunywa chai hata hivyo ana kazi za kufanya. Nataka kuzungumza na wewe hapa mpenzi.”

Nilimtazama tu mke wangu, nina mjua ni mtu wa nyodo. Kukaa hapa na mama Babuu hata asingesema kitu asingependa tu kwasababu haijawahi kuwa. Kitu ambacho naona familia nyingi hata kwetu pia yaani sijui inakuaje.

Β 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata