LOML | Love Of My Life (47)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:47
Nilijifunza upendo kwa familia ya Willy. Wanaishi vizuri sana. Nilitamani na mimi nianzishe utaratibu huu kwangu. Lakini hata mama Babuu mwenyewe ni wazi hawezi isitoshe wanajuana wao.

Lakini Labda mimi sasa ndiyo sielewi, mkiishi kama familia na kula mezani pamoja kuna shida gani?, haibadilishi wala haiharibu kitu zaidi ina dumisha upendo ndani ya familia na mnaishi na furaha pamoja.Sio mke wangu, kazΔ± za nyumbani hizi sio mambo yake kabisa.

Nilianza kula, vile naanza tu simu yangu iliita. Alikuwa ni Willy, nilipokea simu nikitabasamu na kusema β€œkaka!!, kaka!!, niambie ndugu yangu.”
Willy alisema β€œLeo umefurahi sana, unaendeleaje?”
Nilitabasamu na kusema β€œsalama kabisa kaka, tutaongea usijali.”

Akaniambia kWa ucheshi β€œHakuna shida msalimie shemeji yangu.”
Nilimtazama mke wangu na kusema β€œHakuna tatizo nitamsalimia na ipo siku nitamleta.”

Willy alisema β€œnitafurahi sana kusema kweli karibuni sana.”
Nilimjibu kWa uchangamfu β€œnashukuru sana. Karibu.”

Nilikata simu, mke wangu alinitazama na kuniuliza β€œni nani mume wangu?”
Kwa kifupi tu nilimjibu β€œrafiki yangu.”
Halafu niliendelea kula, nilikula na alinitazama na kusema β€œMume wangu tafadhali usiwe hivi.”

Nilimtazama na kusema β€œGabriella tafadhali unaweza kuacha kusisitiza. Nitakuwa sawa, nitakuwa sawa unatakiwa kujua sijisikii vizuri unanielewa.”

Mke wangu alinitazama tu na Kisha kwa upole aliinuka. Nilijua tu amenuna na anavyo penda kudeka lakini kiukweli siwezi kujilazimisha kuwa nina furaha wakati ninaugua ndani kwa ndani. Hivyo nilimuacha aende

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIBOKO YANGU FULL

BIOLOGY TEACHER FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

SHEM MI NATAKA FULL