LOML | Love Of My Life (49)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:49
Unanifanyia nini sasa, tunaenda wiki ya tatu sasa hunigusi, hunitamani, huniitii hata mke wangu. Ni Kama unaishi na mdogo wako au dada yako. Mimi ni mke wako, tumboni nina mtoto wako.

Kwanini unanifanyia hivi sasa, kwanini hunigusi, ina maana bado nakutia kinyaa, nakuchefua kama ni hivyo başı siwezi kukulazimisha tena. Nipe adhabu unayotaka kunipa, ni bora nitajua sina mume kuliko namna hii.

Unanitesa kihisia unafikiri sasa mimi nikapate wapi mapenzi. Sio mimi wala mtoto hakuna anayehisi uwepo wako. İpi hapa kama kivuli tu, nimechoka, nimechoka, ndiyo nilikukosea, nikaomba msamaha nisikukose maishani lakini naona hunielewi kabisa, msamaha wangu unaniumiza kila siku. Nimefanya kila kitu kama mwanamke lakini bado, inatosha sasa, nimechoka mimi, nimechoka sana.”

Mke wangu akachukua shuka lake na simu yake akatoka nje ya chumba hiki akilia. Kusema ukweli nilijisikia vibaya hata na mimi niliona nimezidi kweli ameniomba msamaha. Inabidi tu nianze upya.

Mbona nina hukumu vibaya. Hata kanisani sijaenda kabisa kisa kujiona sifai. Laiti kama Mungu angekuwa ana hukumu hivi hali isingekuwa hivi kwa sisi binadamu.

Sasa kwanini mke wangu ameniomba msamaha, amefanya kila kitu ananifanyia kila kitu nashindwa msamehe. Nahitaji kubadilika, natakiwa kuanza maisha yangu vizuri na mke wangu.

Ndoa ndiyo kwanza inaenda miezi miwili na mimba ya mke wangu itanihitaji zaidi kadri inavyozidi kukua. Natakiwa kubadilika na kuyaacha mambo yapite.Niliinuka kumfuata mke wangu, nilipofika mlangoni nikasikama na kusema “hayupo sawa nimuache kwanza nitamfuata.”
Nikarudi zangu kitandani, si ndiyo usingizi ukanichukua na kuacha mke wangu alale nje ya chumba chetu cha ndoa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata